Taarifa ya makubaliano toka kwa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki imetolewa leo Ikulu Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha Mkutano wa siku mbili wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya hiyo ambapo baadhi ya maadhimio waliyokubaliana ni kwamba Rais Museveni wa Uganda awe msimamizi wa juhudi za upatanishi wa makundi nchini Humo.

Akizungumza wakati wa Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Richard Sezibera alisema kuwa Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni apewe jukumu la usimamizi katika kupatanisha makundi nchini Burundi, pia  Serikali ya Burundi iwanyang'anye silaha kikundi cha vijana cha Imbonerakure pamoja na makundi mengine ya vyama vya siasa ambayo yanamiliki silaha hizo, Umoja wa Afrika (AU) ipeleke waangalizi wa kijeshi kuhakikisha kuwa vikundi hivyo vinanyang'anywa silaha hizo, Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu kutuma Timu ya Wakaguzi na Wataalam wa mambo ya intelijensia kujua kama FDLR wapo nchini Burundi.

Sezibera aliongeza kuwa Upande wowote utakaoshinda uchaguzi unapaswa kuunda Serikali ya Kitaifa ambayo itashirikisha Vyama vilivyoshiriki pamoja na vile visivyoshiriki uchaguzi nchini humo, pia upande wowote utakaoshinda uchaguzi uheshimu makubaliano ya Arusha na kuhakikisha kuwa hautobadili Katiba ya nchi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...