JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAHAKAMA
    Tunapenda kuutaarifu Umma kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (United Nations) Mhe. Ban Ki-moon tarehe 16 Machi, 2015 alimteua Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania kuwa Mwenyekiti wa jopo huru la wataalamu wa kutafuta ukweli zaidi juu ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Hayati Dag Hammarskjöld, kifo hicho kilichotokea kwenye ajali ya kusikitisha ya ndege mnamo tarehe 17-18 Septemba, 1961 maeneo ya Ndola, Zambia wakati akitafuta suluhu ya mgogoro wa wakati wa vita vya Nchi ya Congo (DRC).

Pamoja naye jopo hilo lilikuwa na wajumbe wawil Bw. Kerryn Macaulay wa Australia and Henrik Larsen wa Dermark.  Kazi hiyo iliyochukua miezi mitatu imekamilika na kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu, Ban Ki-moon ambaye pia ameiwasilisha kwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Taarifa kamili ya ripoti hiyo inapatikana kwenye tovuti ya Umoja wa Taifa ya http://www.un.org/dous/journal/asp/ws.asp?m=a/70/132. Aidha taarifa ilitolewa kwenye vyombo vya habari ya tarehe 6 Juni, 2015, inapatikana  kupitia tovuti
Mahakama, tunachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu kwa uwakilishi  wa Mahakama na Nchi yetu na kazi iliyotukuka na kumtakia heri na mafanikio zaidi.

H. A. Kattanga

MTENDAJI MKUU
MAHAKAMA YA TANZANIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...