Shangwe na burudani za kutosha zinatarajiwa kufanyika katika sikukuu ya Eid hapo kesho mkoani Tabora panapo majaaliwa ya Mwenyezi Mungu. Mashabiki mjini Tabora watarajiwa kufurahia onesho hilo katika maeneo mawili tofauti ambapo mchana itakuwa Bwalo la Polisi kuanzia saa 8 mchana na Usiku katika viwanja vya Muungano Mesi kuanzia saa 2 usiku.
Wasanii wa kila nyanja wametua mjini hapo na kufanya mahojiano CG Fm Redio leo mchana; wasanii hao ni Kassim Mganga a.k.a tajiri wa mahaba, Ommy Dimpoz, Mkude Simba (Kitale) na rafiki yake Stan Bakora, Young Killer, na Baraka Da Prince.
Kassim Mganga akiwa CG Fm Redio, 89.5 The point of no Return
Ommy Dimpoz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...