
Bendi ya muziki wa dansi ya African Stars “Twanga Pepeta’ itafanya maonyesho maalum mwishoni mwa mwezi huu yaliyopewa jina la juzi, jana na leo.
Katika maonyesho hayo, bendi hiyo itapiga nyimbo zao maarufu katika albamu zake kuanzia "Kisa cha Mpemba" mpaka albamu ya mwisho kuzinduliwa ijulikanayo kwa jina la "Nyumbani ni Nyumbani".
Pia itapiga nyimbo zake mpya ambazo bado hazijaingia kwenye albamu.
Mratibu wa onyesho hilo, Nasib Mahinya alisema kuwa onyesho la kwanza litafanyika kwenye ukumbi wa Escape One ambapo onyesho la pili litakuwa Agosti Mosi kwenye ukumbi wa Dar West, Tabata na la tatu AGosti 2 kwenye ukumbi wa TCC, Chang’ombe.
Mahinya alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya maonyesho hayo ni kuwakumbusha mashabiki wao wapya na wa zamani, wapi walianzia na walipo sasa. Alisema kuwa wanajua kuwa mpaka sasa kuna mashabiki wa bendi hiyo hawazijui nyimbo zao za zamani.
“Bendi kwa sasa ipo kambini kujiandaa na maonyesho hayo yaliyodhaminiwa na Salut5, CXC Africa, Astery Insurance, EF Outdoor, Master’s club na Clouds Media group, hii ni fursa pekee kwa mashabiki kuona shoo za zamani, ungo, mchi nayo itakuwepo,” alisema Mahinya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...