Mgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Bukoba Bi. Antu Mandoza(Kulia) akirejesha Fomu ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana Bukoba katika ofisi za umoja huo Mjini Bukoba, ahaidi kuinua Vijana Kiuchumi endapo atapata nafasi ya kuwa Mbunge wa Vijana.(Habari Picha na Faustine Ruta/bukobasports).Mcheza kwao hutunzwa, Vijana wazidi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi. Binti Antu Mandoza mwenye kuonekana kuwa na umri miaka 22-25 Amerudisha Fomu za kuwania nafasi ya Ubunge Vijana Viti Maalumu kupitia CCM. Kwa Mahojiano mafupi ameongelea jinsi anavyopanga kuinua Maisha ya Vijana kwa kuwatengenezea Fursa na mbinu mbalimbali za kujiajiri pia kuwaonya kutokukubali kutumika vibaya na MAKUNDI ya Kisiasa tunapoelekea Uchaguzi kwani ni wajibu wetu Vijana kuilinda Amani yetu. Mgombea huyo pia amesema kuwa shauku yake kubwa ni kuwatumikia Vijana kwa kutatua changamoto ya Ajira na pia ametoa ahadi ya kushirikiana na Vijana bega kwa bega kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kagera.
Binti Antu Mandoza akiweka sawa Kumbukumbu zake katika kitabu mbele ya karani Bi. Jasinta Benedicto wa Umoja wa Vijana Kagera.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2015

    Nahisi kama taswira/heshima ya ubunge ishapotea...Mtu ni mtu anachukua form ya ubunge...sasa imekuwa Kuwa kuwa Class representative ni ngumu yahitaji sifa zaidi kugombea kuliko ubunge. Na hii ni kutokana na kuonekana kuwa wanaogombea ubunge na kupewa hivyo viti hawana sifa za kuwa wabunge....Kwani hata kujisimamia mwenyewe ktk kuiheshimu status yake binafsi hawezi ila ubunge anaweza kuwa mbunge....UBUNGE USHAKUWA DILI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...