Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Dk. Seif Rashid (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya Wazazi Nipendeni awamu ya pili katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo mchana. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Anna Bodipo Memba na wa pili kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magema.
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Anna Bodipo Memba (kulia), akitoa hutuba yake kwenye uzinduzi huo.
Mshauri wa masuala ya Afya ya Jamii kutoka Taasisi ya HBC, Mdadike Thabit (kulia), akimuelekeza jambo mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya watoa huduma kabla ya kufanyika uzinduzi huo.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...