Vijana wa Tarafa ya Puge wilayani Nzega wameaswa kuzingatia vigezo wanapokuwa wanaomba mikopo ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ulio chini ya Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo.

Hayo yalisemwa na Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bi.Amina Sanga alipokuwa akitoa elimu ya mfuko wa Maendeleo ya Vijana kata ya Puge leo hii.

“Vijana mzingatie sana vigezo wakati wa kuomba mikopo hii kutoka mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwani bila ivyo mtaishia kukosa izi pesa kila wakati mnapoandika andiko la Mradi.Lazima uwiano wa mkopo na mradi wenyewe uendane,iki ni kigezo kimojawapo muhimu pamoja na swala la umri ambao ni miaka 15-35”,Alisema Bi.Sanga.

Aidha Mkurugenzi msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Bi.Esther Riwa aliwahimiza vijana hao kuijua Sera ya Maendeleo ya Vijana kwani ndio mwongozo wao kwa maisha ya sasa katika kuwaletea maendeleo uku akibanisha kuwa mafanikio pia yapo katika kuanzisha vikundi mbalimbali vya ujasiriamali.

Kwa upande wake Afisa Ushirika wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Bi.Odilia Kimasha aliwaasa Vijana kufanyia kazi mafunzo haya mara moja kwa kujiunga katika SACCOS ya wilaya katika vikundi ili kuanza kununua hisa na kujiwekea akiba ili waanze kukopa.

“Vijana tunawaomba baada ya mafunzo haya mhamasike na kutuona ili mjiunge na SACCOS yetu mkiwa katika vikundi na kuanza kujiwekea akiba ili muendeleze miradi yenu na ivyo vipato vyetu vitakua maradufu”aliongezea Bi.Kimasha.

Nae kijana wa Tarafa ya Puge Bi.Devotha Boniface aliishukulu Serikali kwa kuwakumbuka na kuwapa mafunzo hayo kwani yatawatoa katika dimbwi la umaskini.

Ujumbe kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo upo Wilayani Nzega mkoa wa Tabora ukihamasisha Vijana na kutoa mafunzo ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana,Stadi za maisha,Uongozi Bora na Ujasiriamali.
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bi.Amina Sanga akiongea na Vijana wa Tarafa ya Puge wilayani Nzega(hawapo Pichani) kuhusu mfuko wa Maendeleo ya Vijanana jinsi gani wanaweza kuutumia ili kujipatia fedha za mkopo zenye masharti nafuu na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Afisa Ushirika kutoka Halmashauri ya wilaya ya Nzega Bi.Odilia Kimasha akiwapa elimu juu ya SACCOS zinavyofanya kazi na umuhimu wa kununua hisa kwa Vijana wa Tarafa ya Puge wakati wa programu ya uhamasishaji na mafunzo kwa Vijana inayoendelea wilayani Nzega yakiendeshwa na Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Uratibu na Uhamasishaji kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bi.Esther Riwa akiwauliza swali Vijana wa Tarafa ya Puge juu ya Sera ya Maendeleo ya Vijana ambao ni Mwongozo namba moja uku akiwasisitiza Vijana hao kufanya maendeleo kupitia Miradi.
Mkuu wa kituo cha Vijana Sasanda,mbeya Bw.Laurean Masele akifanya majadiliano na kijana na kijana wa tarafa ya Puge wakati akiwafundisha juu ya kuwa viongozi Bora katika jamii yao na vikundi vyao vya Ujasiriamali uku akisisitiza kuunganisha jamii wanazoziongoza na kuweka mikakati katika kutatua matatizo ya vikundi vyao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...