Na Monica Mutoni
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) wameandaa mafunzo ya hali ya hewa kwa kutumia modeli ya PRECIS (Providing Regional Climates for Impact Studies) kuanzia tarehe 29 Juni hadi 03 Julai 2015. 
Warsha/ mafunzo haya yameandaliwa na TMA chini ya mwamvuli wa mradi wa GFCS unaotekelezwa kwa upande wa Afrika katika nchi za Tanzania na Malawi.  
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka TMA na Kurugenzi ya Hali ya Hewa ya Malawi wanategemea kujifunza matumizi ya modeli ya PRECIS kutoka kwa mtaalamu kutoka Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza ambayo imekuwa ikitumia modeli hiyo katika utekelezaji wa huduma za hali ya hewa. 
 Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa wa utoaji huduma za hali ya hewa pamoja na kuweza kutoa taarifa sahihi za muda mrefu zenye kuweza kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi. 
Alisema Dkt.Kijazi PRECIS ni mfumo unaweza kutoa taarifa za hali ya hewa za muda mrefu (Klimatolojia) kwa eneo husika.
 Mkufunzi wa warsha kutoka Ofisi ya Hali ya Hewa Uingereza bw. David Hein akiendesha mafunzo kwa wanawarsha. 
 Baadhi ya wanawarsha kutoka Malawi na Tanzania wakati wa warsha ya kisayansi kuhusu huduma za hali ya hewa kupitia modeli ya ‘PRECIS’.
 Dkt. Agnes Kijazi akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa warsha ya kisayansi kuhusu huduma za hali ya hewa kupitia modeli ya ‘PRECIS’.
 Wanawarsha kutoka Malawi na Tanzania wakati wa warsha ya kisayansi kuhusu huduma za hali ya hewa kupitia modeli ya ‘PRECIS’.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...