WASANII nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba katika mifuko mbalimbali ya jamii kwa kuwa kufanya hivyo kuna kumuhimu mkubwa katika maisha yao baada kuwa wamestaafu kazi zao au wanapokuwa hawana tena uwezo wa kufanya kazi.

Hayo yalisemwa na msanii mkongwe wa maigizo hapa nchini Bakari Mbelemba maarufu kwa jina la Mzee Jangala wakati akizungumza katika Jukwaa la na Sanaa lililofanyika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mwanzoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam.

Mzee Jangala alikuwa akijibu hoja iliyotolewa na msanii Christian Kauzeni ambaye alitaka kujua ni kwa nini wasanii wakongwe wengi wanakuwa na maisha magumu licha ya kuwa walifanya kazi nzuri zilizo wahengea umaarufu mkubwa hapa nchini.

Alisema wasanii wengi wakonge hawakuwa na utaratibu wa kuweka akiba, lakini kwa sasa kuna mifuko mingi na mifumo mingi ya kujiwekea akiba hivyo ni muhimu kwa sanii kujiwekea akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza alisema huu si wakati wa msanii kupata shida baada ya kustaafu au kuzeeka kwa kuwa kuna mifuko mingi ya kuweka akiba na hata ya huduma za afya ambayo kwa mchango kidogo inatoa unafuu mkubwa wahuduma.

“Haipendezi kwa msanii aliyekuwa na jina kubwa au umaarufu katika nchi anapokuwa amepatwa na maradhi kusubili harambee ipite ili apate matibabu, msanii akijiunga na mfumo wa bima ya Afya kwa mfano NHIF analipa fedha kidogo sana na anapata uhakika wa matibabu kwa muda mrefu wa maisha yake,” alisema Mngereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...