Baadhi ya Wanalyalamo wakijumuika na watoto wa 
kituo cha Yatima Group Trust Fund kilichopo Chanika, Dar es Salaam
.

baadhi ya wanalyamo family katika picha ya pamoja na mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho, Winfrida Lubanza(mwenye miwani na blauzi nyeusi)

WITO umetolewa kwa Watanzania nchini kujitolea kwa hali na mali usaidia watu wenye uhitaji ikiwemo watoto yatima wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali. Wito huo umetolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Yatima Group Trust Fund kilichopo Chanika, jijini Dar es Salaam, Winfrida Lubanza wakati akizungumza na wanafalia wa Lyalamo.

Alisema jamii inapaswa kuwakumbuka na watoto wakuopo katika vituo hivyo kwani wanastahili kupata mahitaji muhimu ya kibinadamu kama ilivyo kwa watoto waliopo majumbani. "watoto yatima ni watoto km wengine nao wana uhitaji sawa hivyo jamii isiwasahau na kwani nao wanapata furaja na kupata matumaini zaidi,"alisema.

Aidha, aliongeza kuwa kituo chake kinakabiliwa na chsnggamoto mbalimbali ikiwemo chakula, madawa, sabuni na ada kwa wanafunzi sambamba na mtaji wa kuwezesha kuanzisha biashara ambayo itaweza kuwapatia pesa za kujikimu.
"tunachangamoto nyingi mfano kuna mwanafunzi yupo kidato cha nne amerudishwa kituoni sababh hatujakamilisha ada,"alisema.
Naye kiongozi wa Lyalamo family, Aziza Kibwana alisema wamefarijika kufika kituoni hapo na kuona vhangamoto hivyo watajitahidi kuchangia walichojaaliwa.Pia amesisitiza wadau kujitokeza kusaidia. " Sisi tumesoma shule ya msingi boarding tukiwa wadogo na tulikuwa na watoto kutoka katika vituo kama hivi hivyo tunaguswa sana na hali zao ndio maana tuko hapa," alisema.Aziza aliongeza kwamba kupitia umoja wao watajitahidi kadiri wawezavyo kuvifikia vituo mbambali na kutoa misaada.
" Humu kuna marais, kuna mawaziri, wabunge, wanasoka, wasanii, wafanyabiashara, madaktari, wahasibu n.k sasa ni muhimu kuwakumbuka na watoto waliopo huku ili kuwajengea misingi mizuri ya kutimiza ndoto zao," aliongeza .Katika ziara yao Lyalamo family walikabidhi kituoni hapo vyakula, mafuta, dawa, madaftari, sabuni na vitu vinginevyo ambapo watoto waliopo kituoni hapo walifurahi na kushukuru.
Kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2001 kinalea watoto kati ya 150 hadi 300 wenye umri wa kuanzia 0 hadi miaka 18.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...