Mwenyekiti
wa Kikundi cha Tujiajiri Group cha Tarafa ya Nyasa wilaya ya Nzega Bw.Fanuel
Kifunyu(waKwanza kulia)akiongea na kuonyesha ujumbe kutoka Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuhusu Bidhaa mbalimbali wanazotengeneza
zikiwamo Sabuni,matofali ya kufungamana,na karanga baada ya kupata mafunzo ya
mfuko wa Maendeleo ya Vijana,Stadi za Maisha,Ujasiriamali na Uongozi Bora.Wengine
pichani ni Afisa Vijana Laurean Masele(wa pili kutoka kulia),Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Uratibu na Uhamasishaji(katikati) na
Afisa Vijana Amina Sanga(Mwenye kiremba cha Njano.
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Uratibu na Uhamasishaji Bi.Esther Riwa
akimwuliza maswali Mwanakikundi cha Ushonaji na utengenezaji wa Viatu Bw.Chepe
changamoto gani wanazokutana nazo katika ufanyaji wao wa kazi za ushonaji uku
mwanakikundi uyo akibainisha kutopatikana wa mashine za kutengenezea viatu ivyo
mpaka nchi jirani ya kenya.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana
Uratibu na Uhamasishaji Bi.Esther Riwa(wa Kwanza kushoto) akipita katika shamba
la nyanya la kikundi cha Nserema kinacholima Nyanya,Matikiti,na Kabeji
kutoka kijiji cha Iyombo Tarafa ya
Nyasa.kikundi icho kinategemea kuomba mkopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana ili kuboresha kilimo chao kwa kununua pembejeo za kilimo,kununua mbegu
bora na madawa ya kuulia wadudu.katikati mwenye shatu jekundu ni Mwenyekiti wa
kikundi icho Bw. Stephen Ndikamara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...