Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Sweden hapa nchini ambaye amemaliza muda wake wa kazi, Mhe. Lennarth Hjelmaker. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Balozi wa Sweden anayemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Lennarth Hjelmaker akimsikiliza Balozi Kasyanju (hayupo pichani) wakati akitoa hotuba ya kumuaga Balozi huyo. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine.
Balozi Sokoine akizungumza kuwakaribisha Wageni waalikwa kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Sweden aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Balozi Hjelmaker nae akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa kumpatia ushirikiano mkubwa katika kipindi chote cha miaka mitano aliyokuwepo hapa nchini kama Balozi wa Sweden
Picha ya pamoja
Balozi Kasyanju akiagana na Balozi Hjelmaker mara baada ya hafla ya kumuaga kukamilika. Picha  na Reginald Philip
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...