Ukiwa na haraka Mbweni JKT jiandae kupiga mbizi
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UPIGE mbizi,Ndivyo unavyoweza kusema msemo huu kama
unahitaji kupita haraka haraka katika eneo la Mbweni JKT, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, mahala panapojengwa
daraja la kuvukia watu kwa miaka mitatu sasa, halina dalili za kukamilika hivi
karibuni.
Ni eneo tata,Ni eneo linalokera na kusumbua watu mno, Mbaya
zaidi, ni eneo lililozunguukwa na majumba ya watu wenye ukwasi au ukubwa wa
majina ya viongozi waliojenga katika eneo hilo. Eneo linalojengwa daraja hilo
ni kwenye mkondo wa maji unaotokea baharini.
Gari likivuka eneo la mkondo wa bahari, ambapo pia ndipo panapojengwa daraja hilo hatua chache mkono wa kulia kutoka gari linapopita, Maji yakijaa hapo hakuna kupita wala kuvuka.
Kwa wanaofahamu tabia za mkondo huu wa bahari watakuwa wanaelewa, Na wasiofahamu ni kwamba, linakuwa na tabia za kujaa maji na kupungua kila wakati. Kwa mfano, mtu anaweza kupita saa tatu asubuhi akakuta hakuna maji mengi. Lakini dakika kadhaa mbele, maji mengi yanajaa kutokea baharini. Ukifanya makosa na ukiwa na haraka ya kuendelea na shughuli zako, ndipo hapo unapopaswa upige mbizi.
Hapa ndipo panapojengwa daraja hili.
Itabidi uyavulie maji nguo ndipo upite, Na ikiwa unagari, huna budi
kusubiri kwanza yapungue kama si kuisha kabisa maji hayo.
Au utafute njia
nyingine za kukufikisha eneo unaloelekea, ingawa njia hiyo inausumbufu mkubwa
wa muda na gharama nyingine pia. Ni kutokana na hilo, serikali kwa kupitia Halmashauri ya
Wilaya Kinondoni, inapaswa kuangalia kwa jicho kuu eneo hili.
Iangalie tatizo ni
nini? Mbona daraja hilo halikamiliki kwa miaka mingi sasa, hakuna kinachoendelea, watu wanapata tabu, Mbaya zaidi ni eneo linalovutia na kusisimua, maana
haiwezekani mtu kujenge nyumba kwa mamilioni ya pesa wakati njia ya kumfikisha
kwake haieleweki eleweki.
Ni wazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni pamoja
na DC Paul Makonda wanapaswa kuliangalia suala hili kwa kina.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...