Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisisitiza jambo wakati akifungua Maonyesho ya 5 ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Young Scientists Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha akimtambulisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa Balozi wa Kenya nchini Tanzania Chirau Ali Mwakwere kabla ya kufungua maonyesho hayo mwishoni mwa wiki.
Na Daniel Mbega wa brotherdanny.com
RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, amewataka walimu katika shule za msingi na sekondari kutumia lugha ya Kiswahili kufundisha sayansi, kwani lugha hiyo inaeleweka vizuri.
Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Tano ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini jijini Dar es Salaam jana, Alhaj Mwinyi amesema Kiswahilini lugha inayoeleweka vizuri, si kwa wanafunzi tu,bali hata kwa watu wengine, hivyo ni vyema walimu wakaweka mkazo katika kuitumia kwenye masomo ya sayansi.
“Nimepita kwenye maonyesho haya, baadhi ya wanafunzi walikuwa wananiuliza ‘tukueleze kwa Kiswahili au kwa Kiingereza’, nikasema tumieni lugha yoyote tu. Wengine wamenieleza Kiingereza na wengine Kiswahili.

Balozi wa Kenya nchini, Chirau AliMwakwere (wa pili kushoto) na Balozi wa Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan wakisikiliza kwa makini maelezo ya wanafunzi walioshiriki maonyesho hayo. Nyumaya Balozi Gilsenan ni Dk. Gosbert Kamugisha, Mkurugenzi Mtendaji wa Young Scientists Tanzania.
BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI
BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI
sivibaya kutumia lugha yetu kwenye sayansi lakini nafikiri tutarudi nyuma badala ya kwenda mbele kwa mtazamo wangu , kutafsiri vitabu vyote vya kiingereza ktk kiswahili sio kazi ndogo , kitaaluma tutaachwa nyuma kwa kuwa sisi hatuna uwezo kifedha kuendesha tafiti kwa hio itabidi tuende kwenye mikutano nje ambako kiingereza ndio lugha ya mawasiliano , tusiangalie wachina ,wajapani , warusi wajerumani nk kwamba wao hawatumii kiingereza lakini wao wanauwezo wa kutafiti mambo ambao sisi hatuna , huu ni wakati wa kuimarisha kiingereza kuanzia shule za msingi kama tunataka tuende na wakati , vinginevyo tuendelee kama tulivyo , kosa hili alilifanya mwl nyerere mwanzo na ndio mpaka leo sisi hatujui kiingereza wala kuandika na tumebaki nyuma
ReplyDeleteNdugu madawa sio kujua Kingereza ndio kujua kila kitu...Kiswahili ni lugha na inawezekana... Mimi naongea Kiswahili Kingereza Kijerumani na Spanish, Mjerumani anatafiti kwa kijeru na sokoni anatumia English.
ReplyDelete