Mratibu
wa Bima kutoka Bayport Financial Services, Ruth Bura, katikati
akizungumza katika uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Magari, pikipiki
na Bajaj kwa kushirikiana na Kampuni ya NIKO Insurance. Kulia ni Meneja
Uendelezaji wa Biashara wa NIKO Insurance, Jabir Kigoda na kushoto ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa Niko, Mannaseh Kawoloka.
Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamTAASISI
ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya
mikopo, imezindua huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj,
ikiwa na lengo la kurahisisha masuala ya usafiri kwa wateja wao ili
kukwamua zaidi. Kuanzishwa
kwa huduma hiyo mpya kumetajwa kuwa kutachangia kwa kiasi kikubwa
wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri waliokuwa wakishindwa kulipa bima
kwa wakati na wakati mwingine mteja kupata ajali hali ya kuwa hana
huduma ya bima inayoweza kumlinda.
Oparesheni
Meneja wa Bayport Financial Services, Charles Mgeta, kushoto
akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Magari,
pikipiki na bajaj. Anayefuata ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NIKO Insurance,
Mannaseh Kawoloka.
1. Afisa
Mtendaji Mkuu wa NIKO Insurance, Mannaseh Kawoloka katikati akizungumza
jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na
bajaj inayoendeshwa na Taasisi ya Bayport Financial Services. Kulia
kwake ni Mratibu wa bima hiyo, Ruth Buran a kushoto kwake ni Meneja
Oparesheni wa Bayport, Charles Mgeta. Picha zote na Mpiga Picha Wetu. 
Wakati
shughuli ya uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na
bajaj kutoka Bayport Financial Services kwa kushirikiana na NIKO
Insurance ukiendelea Makao Makuu ya Bayport leo asubuhi.
Meneja
Madai wa Niko Insurance, David Mshuza, akiafuatiwa na Cecilia Peter na
Lester Chinyang'anya. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.
Akizungumza
leo asubuhi jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Bima hiyo kutoka Bayport
Financial Services, Ruth Bura, alisema huduma yao wanayoshirikiana na
NIKO Insurance ina lengo kubwa la kumrudisha mteja wao (mkata bima),
katika hali aliyokuwa nayo kabla ya kupata ajali hiyo.
Alisema
mara kadhaa baadhi ya Watanzania wamekuwa wakikimbizana na askari wa
usalama barabarani kwa sababu hawana bima kwenye vyombo vyao vya
usafiri, ila kwa kupitia huduma yao mpya, sasa kila mtu anaweza kujiunga
na bima kwa njia rahisi, wakiamini kuwa ni sehemu yao ya kuhakikisha
wateja wao wanakuwa kwenye usalama ili watimize wajibu wao kufanya kazi
na kukuza uchumi wao na wa Tanzania kwa ujumla.
“Ili
mtu aweze kujiunga na huduma yetu ya Bima kutoka Bayport Financial
Services, kwanza anatakiwa kujaza fomu yetu ya mkopo na ile fomu ya
udhibitisho wa bima, bila kusahau nyaraka za umiliki wa gari lake ili
tujiridhishe na umiliki wake.
“Baada
ya hapo, gari lake litapigwa picha tano kila pembe, ikiwa ni nyuma na
mbele na kwenye injini na tukimaliza hatua hiyo, mteja wetu atapatiwa
mkataba wa bima pamoja na ‘sticker’ kuonyesha kuwa yupo kwenye bima,
huku huduma hiyo ikiwa ni rahisi kwa sababu gharama za bima kwa mwaka ni
kuanzia Sh 354,000 pamoja na VAT,” Alisema.
“NIKO
tunajisikia faraja kubwa kushirikiana na wenzetu Bayport Financial
Services kutoa huduma bora na kiwango cha juu, hususan kwa kupitia
huduma hii mpya ya bima ya magari, tukiamini kuwa itawafanya Watanzania
wote watembee kifua mbele, maana ile presha ya kukimbiana na watu wa
usalama barabarani itakuwa imepatiwa ufumbuzi,” alisema Kigoda.
Bayport
Financial Services ni taasisi ya kifedha inayotoa huduma mbalimbali za
mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa, bila kusahau mradi wa mikopo ya
viwanja vya Vikuruti unaoendelea na kuwafanya Watanzania watembee kifua
mbele, huku taasisi hiyo ikifanikiwa kuwa na matawi 80 Tanzania Bara,
hivyo kutoa huduma bora na kwa njia rahisi kwa kupitia matawi yao au
mtandao wao wa www.kopabayport.co.tz.
Naye
Meneja Uendelezaji wa Biashara wa NIKO Insurance, Jabir Kigoda, alisema
kuwa huduma hiyo ni nzuri na rahisi inayoweza kuwanufaisha wateja na
Watanzania wote, hivyo wanapaswa kuichangamkia ili kuwaweka katika
usalama wao na wa vyombo vyao vya usafiri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...