Baada ya kura kutotosha kumfanya apite katika kura za maoni kugombea Ubunge kwa viti vya Vijana mkoani Tabora, Zahara Muhidin Issa Michuzi (pichani) amepokea matokeo kwa moyo mkunjufu na kumpongeza mshindi Irene Uwoya na kumuahidi ushirikiano katika mambo yote mema ya kuendeleza vijana mkoani humo.
Zahara ambaye sasa ataelekeza nguvu zake katika kusaka digrii ya pili ya uchumi, amesema kwamba anawashukuru wajumbe wa mkutano wa uchaguzi, baba yake, mama walezi, kaka Mkala Fundikira wa Tanzania Bloggers Network (TBN) kanda ya Magharibi na wana TBN wote wa ndani na nje ya nchi akiwemo kaka Jeff Msangi wa Canada na Mubelwa Bandio na DJ Luke wa Marekani, wanahabari wote wa makundi ya Whatsapp chini ya Francis Godwin na walimu wake pamoja  na wananchi wote kwa ujumla kwa kumpa heshima ya kumuunga mkono kwa kujitokeza kujaribu kuomba nafasi hiyo.
Amesema kushindwa kwake hakumaanishi lolote zaidi ya kwamba demokrasia imechukua mkondo wake na aliyehitajika kuendeleza mapambano amepita na yeye hana kinyongo naye na ataendelea kuutumikia mkoa wa Tabora  katika nafasi yake ya mtu ambaye si kiongozi.
Zahara ametoa mwito kwa wagombea wa nafasi zote kwamba kushindwa ni moja ya matokeo katika ushindani wowote hivyo ipo haja ya kujenga utamaduni wa kukubali matokeo bila ya hasira ama kinyongo kwani dunia i duara, na kwamba mlango mmoja ukifungwa kuna mwingine utafunguka.
Amesema hana mpango wa kuhama CCM ambayo anaiamini kuwa ni chama ambacho kitaenzi na kutunza hadhi na mustakabali wa Taifa la Tanzania kuliko chama chochote.
"Kushindwa kwangu kupata kura za kutosha sio mwisho wa dunia. Nina imani kwamba wapiga kura walijua wanachokifanya. Mimi ni nani kuwaoneshea kidole?  Maisha yaendelee kama kawaida na Mola awajaalie wote kwa yote" alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa


  1. SALUTE!, that is a required spiriti. Leave the fight for tomorrow... (uthiame thithiem michepuko thio dili)

    ReplyDelete
  2. Huu ndiyo ukomavu wa kisiasa na busara katika ushindani! Kura zisipotosha kwako, unampogeza aliyekushinda na maisha yanaendelea kikawaida. Lakini kwa upande mwingine huyu Binti yetu bado mdogo sana na hivyo nafasi bado ipo kwake.... aendelee tu kujijenga ndani ya chama na siku moja atapata nafasi ya kuwatumikia wana-CCM & wa-Tanzania kwa ujumla wake.

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na mtoa maoni no. 2 hapo juu. Kwa kweli ni kitendo cha ujasiri kuthubutu, kujaribu na kukubali kuyapokea matokeo katika hali yeyote ile (kushinda ama kushindwa). Naamini huo ni mwanzo mzuri na In Sha Allah, penye uhai na uzima ipo siku utatimiza malengo yako, just the matter of time. Endelea tu kujiimarisha na kuwa mshiriki hai ndani na nje ya chama na shughuli zote zihusianazo, hii ni pamoja na kuwatumikia kwa dhati na kwa nia moja wana CCM na watanzania wote kwa jumla bila kuangalia tofauti za aina yeyote zilizopo. Mola akubariki na kukuongoza kila penye kheri na ufanisi mwema huko usoni wendako - Amen.

    ReplyDelete
  4. Usikate tamaa, ni vizuri umejaribu kama kiongozi kijana , fursa za kuongoza bado ziko nyingi ambazo zinaweza kuleta mabadiliko kwa vijana zifuatilie hizo hata katika jukwaa zisizo za kiserikali NGOs. Endelea kuthubutu dada wakati unakuja milango itafunguka..

    ReplyDelete
  5. Roma haikujengwa kwa siku moja hii ni hatua muhimu, nzuri na kubwa umepiga katika safari yako kisiasa tafadhali usirudi nyuma panga mikakati kwa raundi ya pili hata ya tatu wengi walipata shida kama zako katika safari zao za kisiasa lakini baadae walifanikiwa rais Bill Clinton wa marekani alikosa ugavana wa 'state' yake mara ya kwanza baadae akashinda mara mbili na mwisho akawa rais wa marekani kwa hiyo dada yangu jipange vema muhimu uhai inshallah utafanikiwa.

    mdau.

    Mauritius.

    ReplyDelete
  6. Umeaanzq vema daima mwanzo huwa mgumu lakini umethubutu usikate tamaa kuvijinka kwa koleo si mwosho wa uhunzi

    ReplyDelete
  7. Ameanza vema hakuna kukata taama bado ni kijana daima mwanzo huwa mgumu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...