Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Segerea anayemaliza muda wake, Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) nyumbani kwake Segerea mwisho jijini Dar es salaam, wakati akitangaza kujiondoa uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo Jumapili Agosti 2, 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Kimeo hiki hakifai M4c

    ReplyDelete
  2. Kuna haja ya kuchunguza sana haya ya wana CCM wengi kukimbilia Chadema, naona washahisi kuwa watakosa mara hii wanatuma watu wao waende Chadema so hata ikipata Chadema , Sera zitakuwa ni zile zile za CCM

    ReplyDelete
  3. HAYA WAZINDAKI NA WANAFIKI ONDOKENI MAPEMA MTUACHIE CHAMA CHETU . KUMBE NA WEWE NI KAMA KINYONGA UNABADILIKA BADILIKA . MFYUUUUU

    ReplyDelete
  4. jamani hii imekaaje, yangu macho

    ReplyDelete
  5. The mdudu, mtahama sana na tamaa zenu lakini ushindi wa kishindo ni kwa Dr Magufuri na ata wa nyoosha kisawasawa yaani baba aako mzazi anakwambia hufai kwenye hii family yangu coz huna maadiri wewe ndio kwanza unasema na mimi kuanzia Leo wewe sio babaangu lo kichekesho baba atabaki kua baba tu eti na mimi nahamia kwa jirani yangu ndio atakua baba yangu sawa ila ukumbuke huyo ipo siku atakwambia njoo uniogeshe na wewe ukijiangalia ni dume la haja sijui utamjibu vipi? wahama hama mtatia akili safari hii Hongera sana ndugu A, Kinana haya ndio matunda ya kuna mawaziri MIZIGO na ndio hiyo ikikatwa cha kwanza eti mimi na hama chama nenda zako coz Magufuri hawezi fanya kazi na MIZIGO

    ReplyDelete
  6. HONGERA SANA CCM MAANA MCHAKATO WA DODOMA UMESAIDIA KUWATOA HOFU WANANCHI NA KUANZA KUPIGA CHINI MZIGO YOTE, PIA WANAOHAMA WANATUSAIDIA KUPUNGUZA KAZI KATIKA KAMPENI MAANA WOTE WANAKIMBILIA WODI YA MAJERUHI CHADEMA. VP KAMA MNGESHINDA KURA ZA MAONI JE BADO MNGEHAMA NA KUSEMA CCM HAKUNA DEMOKRASIA? SASA BASI HUKO CHADEMA NDIO HAKUFAI KABISA NDIO MAANA DK SLAA MPAKA LEO KAJIFUNGIA NDANI. LOWASA ALIPOCHUKUA FOMU TU ZOEZI LIKAFUNGWA MARA MOJA ILI KUZUIA WENGINE WENYE SIFA ZA KUGOMBEA WASICHUKUE FOMU MAANA WANGEKUJA KUMSUMBUA BAADAE NA MAMBO YA VIKAO VYA MCHUJO NA KUULIZANA KUHUSU RICHMOND NA HILO NA SHARTI ALILOMPA MBOWE KABLA YA KUJIUNGA NA CHADEMA. JE IKO WAPI DEOMKRASIA? AIBU YENU MAMLUKI NA MKAE MKIJUA MAGUFULI NDIE RAIS WA AWAMU YA TANO KWA ZAIDI YA ASILIMIA 70 YA KURA ZOTE ZITAKAZOPIGWA NA WENYE AKILI TIMAMU, NA HAPO NDIO UTAKUA MWISHO WENU KISIASA KWANI CCM INAJIPANGA KUWEKA KANUNI YA KUTAKUWAPOKEA WALIOHAMA CHAMA IWAPO WATAOMBA KURUDI TENA.

    ReplyDelete
  7. Mizigo inajiondoa yenyewe

    ReplyDelete
  8. Mimi ni ex mwalimu niliyewahi kufundisha siasa. Nakerwa na wanasiasa wanaohama vyama baada ya kushindwa kukubalika kwenye vyama vyao na nina imani wanahama kwenye vyama vyao vya kwanza kwa sababu moja tu ya uchu wa madaraka na si kingine kwa sababu ifuatayo
    Unapojiunga na chama ni kwamba unaamini na unaafiki ideology ya hicho chama, ni kama dini unakubaliana na misingi ya kile chama. CCM ilikuwa inaamini siasa ya ujamaa na kujitegema, sijui vyama vingine vinaamini juu ya misingi gani katika kuwalatea maendeleo wananchi, lakini naamini sio imani moja na CCM na ndio maana ni chama pinzani.
    Sasa inakuwaje leo upo chama hiki, kesho cham kile? Au ni ile hadithi ya paka aliyesilimu na akasema yeye ameacha kabisa kula panya, na panya walipoamini ni kweli kasilimu, ndio alipoanza kuwala kisiri bila wao kujua, hadi walipowashtukia wanamalizika na paka aliyeokako ananenepa.
    watanzania tuwaofope kabisa malaya wa kisiasa, hawana wema na maendeleo ya nchi, ila ni kwa manufa ya matumbo yao. Mungu atupe busara tuwajue nia yao kabla ya uchaguzi.
    kila la heri tanzania.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Demokrasia ndiyo hiyo...unatoka CDM unaenda CCM au unatoka CCM unakwenda CHADEMA. Hiyo ndiyo dwmokrasia, itikadi za vyama hazitofautiani sana zote zinalenga kwenye kuleta maendeleo kwa watanzania wote, kinachotofautiana ni njia za kuleta maendeleo ambazo ndizo tofauti lakini malengo ni moja kuleta maendeleo. Ni kama vile makampuni mawili tofauti ya kuleta maendeleo kwa hiyo wanapohama wafanyakazi siyo kwamba hawana mapenzi na mashirika yao au makampuni yao.

      Delete
  9. Wanafiki wa kisiasa hawa, pamoja na kuwa mzigo na kulindwa na mhe. JK Leo anasaliti. Aende zake fisadi mkubwa, msomi Mzima anaburuzwa na mvi. Atoke tubaki na ccm yetu.

    ReplyDelete
  10. Wanakera sana watu waaina hii, wanafuata watu na sio chama. Hawana misimamo, Leo wanaioona cdm safi wenzao wanaikimbia.

    ReplyDelete
  11. Aende zake

    ReplyDelete
  12. Tamaa tu ya madaraka, hatutaki mizigo UKAWA. Nitashangaa CHADEMA wakimpa nafasi

    ReplyDelete
  13. Chadema waangalieni sana hawa jamaa watawaulieni chama..! Huyu jamaa nimemsikiliza kwa makini sana eti anasema hajawahi kuwa waziri ,anadai eti vijana wadogo tu wanakuwa mawaziri yeye anahiyo hiyo nafasi ya unaibu waziri hapandi cheo hahaaaaaa (shame) hivi hili ni jambo la kuongea kwenye press conference kwel????? Hapa kinachotafutwa ni cheo tu wala hakuna kingine

    ReplyDelete

  14. JK alifanya kazi katika mazingira magumu sana, only 2 out of 10 of his cabinet ministers at some time ndio waliyokuwa nae PAMOJA katika FIKRA na utekelezaji. Waliobakia ilikuwa ni kumharibia tu, aonekane hafai.

    Hivyo basi. WOTE ambao hawakumtakia mema JK...w a o n d o k e...ili wabaki wenye fikra MOJA somehow...
    Mfano kama haya mapakacha tunayoyaona yanageukageuka na kuleta ligi ziziso na tija na kuanza kuachia bodi, kweli mabadiliko tutayaona.

    Jinsi UTENDAJI wa JPM ulivyojionyesha, tingatinga...AKIBAKIA na timu ambayo HAIJAKALIA KUMKOMOA like they did to JK, mabadiliko yataonekana.

    Wapo ambao WATAOBAKIA, HAWATAHAMA...wazee wa kazi, yani usalama, wadhibitini hawa, na lie michanga ya macho na tiktaka na mbavu nene kama kazi...

    ReplyDelete
  15. Mbona watu wanahama DINI kila siku - itakuwa CHAMA?
    Mna wasiwasi gani? Au mnataka waje kwenu tu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usiwe kichwa cha mwenda wazimu, kila anayetaka kujifunza kunyoa unamuachia. Usiwe nvivu kufikiri. Hao jamaa ndio lesho watakuwa mawazidi wako, watasaini mikataba isiyoeleweka na iwiyokuwa na misimamo na yenye yumbayumba, kesho yangu kesho kutwa simba, eti ni vile watu wana hama dini hivyo tu a iwashangae hao. Pole ndugu hao ndugu wanaponyoosha mikono kuomba kura zetu ni lazima tujue nia zao.
      Amuka

      Delete

  16. MJADALA SIYO WA KUHAMA DINI WEWE VIPI, TUNALIPA KODI, TUNACHANGIA KUTOA VIONGOZI WATAOTUONGOZA,, RUDI KAJIFICHE CHINI YA JIWE LAKO.

    ReplyDelete
  17. Historia ya Makongoro inaanzia NHC kabla hajaingia kwenye siasa,akiwa shirika la nyumba alikuwa mtu mkubwa sana,yeye na mkurugenzi wake mkuu hawakuwahi kufanya mabadiliko makubwa kwenye shiriki mpaka walivyotimuliwa na kuja NEHEMIA MCHECHU,mnalionaje shirika la nyumba sasa? Kwa hvyo kwangu sishangai huyu mtu kuwa mzigo katika serikali ya kikwete,kumbukumbu zinaonyesha hata uchaguzi wa mwisho uliompa ubunge segerea alifanya magumashi makubwa kwa muda mrefu wana segerea walikuwa hawamtaki coz hana jipya alilowafanyia,kuhama ccm kwake ni halali kwa sababu alikuwa anajua kuwa hana nafasi,visingizio na sababu havina tija wakati huu wewe nenda unakotaka kwenda thats so,iache ccm yetu isonge mbele.

    ReplyDelete
  18. Huyu jamaa feki sana. Nashangaa JK alimweka vipi huyu? udokta wa kufoji msomi gani hajui nafasi ya kuteuliwa ni dhamana si haki! sasa huko CDM atapata uwaziri? nenda salama bana makapi tu!

    ReplyDelete
  19. hivi kukiwa na mkutano wa baraza la mawaziri atahudhuria huyu, na kukaa meza moja na CCM? maana bado ni waziri wa serikali ya CCM , ama atajiuzuru unaibu waziri pia?

    ReplyDelete
  20. Huyu tumsamehe BURE na kumpuuza kabisa yaani hoja ya kuwaeleza watu kweli!. Ama kweli maajabu hataisha huku duniani, yaani kuna wabunge wamekuwa bungeni zaidi yake na wala hawajawahi hata kupewa ukaimu (acting) wachilia mbali unaibu (Deputy) sasa huyui pamoja na priviledges zote hizo bado analeta Uendawazimu uchwara.

    ReplyDelete
  21. Ccm tulieni mbona mnatoka mapovu midomoni,tanzania ni nchi ya kidemokrasia mwache aende anakotaka ni haki yake,mbona na hasira hivyo Kama mmekula nyuki,mbona bado sana,nafurahi kuona demokrasia inakuwa,mfumo dume wa chama kimoja unatokomea,thanks lord.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio suala la CCM au chadema hapa ndugu. Suala no viongozi wababashaji na wananchi wasiojua haki zao. Nuna maana kama huyo unayemshabikia yupo kwebye chama unachokipenda , unafunga macho na masikio, hutafakari? demokrasis au domokrasia, kama alivyosemaga Nyerere? Hamna anayesema kuhusu mfumo dume (whatever that means) au mfumo wa chama kimoja. Tunaongelea viongozi wanaotaka tuwape kura zetu za ndio. Waende bungeni wakatuwakilishe na sie tupate maisha bora ikiwemo ajira, afya na elimu. Ni jukumu letu tukiona wanakosea tuseme, usije ukakaa kimya wakaenda bungeni kuwakilisha matumbo yao tu, halafu ndio tuanze kulalama.
      Hii ndio demokrasia yaanu b kuwa na say katika l ile linalokuhusu, in case you didn't know that.
      Thanks lord

      Delete
  22. CCM shikamooni, nyinyi ni kiboko! Kwanza mmekoboa magamba ya vinyonge kwa kiwavua kwenye kura za maoni. Sasa vinyonga wote waliokobolewa magamba sasa wanabadili rangi zao na kuvaa magwanda na ngozi mpya.

    Safari hii tutayaona mengi.

    ReplyDelete
  23. Gamba hujivua lenyewe halivuliwi.....mbele kwa mbele yatajivua yote yasiyofaa kuwa ndani.

    ReplyDelete
  24. Hhahahaha nimefurahi sana kuona hisia za watu humu. Kiukweli huyu jamaaa alikuwa Mzigo CCM, Mzigo kwa Wananchi na Atakuwa mzigo anakoenda. Nina hakika hata akigombea na Jiwe, Jiwe litashinda. kungekuwa na uwezo wa kumfukuza ubunge huyu wananchi wa segerea wangemfukuza kabisa. Sababu zake za kuhama zinanifanya nijiulize huo unaibu waziri kaupataje. Pole JK uliowaamini ndio hawa. Hongera sana Madam Bona Kalua kwa kutuondolea nuksi katika maendeleo ya Segerea.

    ReplyDelete
  25. Jamani hebu tutofautushe utendaji na utashi. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Ni mzigo, msomi fake, kabebwa...... Yote hayo hayamuondolei haki yake ya msingi kama binadamu mwenye UTASHI na haki ya kuamua atakacho ili mradi tu havunji sheria!
    Hakuna haja wala haki ya kumhukumu kwa maamuzi yake. Time will tell

    ReplyDelete
  26. Chadema sasa wamekua wanachukua makapi yaliyoachwa CCM.MAHANGA Hata term iliyopita segerea alishinda kwa mbinde nani alikua anamtaka!!lol

    ReplyDelete
  27. Angalieni sana wengine ni MAMLUKI

    ReplyDelete
  28. Wewe umesema:MJADALA SIYO WA KUHAMA DINI WEWE VIPI, TUNALIPA KODI, TUNACHANGIA KUTOA VIONGOZI WATAOTUONGOZA,, RUDI KAJIFICHE CHINI YA JIWE LAKO.

    Mimi nakujibu: Kuhama dini na kuhama chama ni sawa. Yote ni maamuzi ya mtu. Yeye alikuwa CCM mkampa madaraka, sasa ameenda upinzani sisi tutampa madaraka. Uamuzi wa kuondoka ni wakwake na yuko huru na uamuzi wa nini apewe huko anakoenda ni wa wananchi husika.

    Ni sawa tu na kutoka dini moja kwenda nyingine, huko unakoenda unaweza kuwa Shehe, Padri au Mchungani kutokana na maamuzi ya hao watu wa hiyo dini yako. Sasa cha ajabu nini. Kama hujaelewa basi wewe akili yako IMEDUMAA kwa fikra za KIZAMANI za chama KIMOJA.

    ReplyDelete

  29. Dini ni Imani. Nimuombe, Anisaidie, Anilinde, Aniokoe, Aniponye. BILA KUMUONA.

    Dini haina sera, ina miongozo, historia, hadithi, sheria, n.k.
    Dini ina amri 10, ambazo HAZIBADILIKI.

    Siasa ni biashara ya NISHATI, BENKI na MAWASILIANO, MEDIA.
    Matatizo yote duniani yanatokana na SIASA ambayo ni mjumuiko wa hayo mambo 3.

    Nakataa ukituambia kuhama dini ni sawa na kuhama chama cha siasa.

    Siasa ni biashara. Sera siyo FIXED, zinabadilika. "katiba siyo biblia"
    Dunia nzima sera 'zinaenda na wakati', zinabadilika. Dunia inabadilika.

    Wakati dini ni FIXED.
    Aliyeumba mbingu na ardhi ni 1 tu.


    UCHAMBUZI NA UKUBALI WA MAMBO HAYA MAWILI NI TOFAUTI. USITUPOTOSHE TUKAICHUKULIA IMANI NI SAWA NA KUTOKA CCM KWENDA CUF AU KUTOKA CHADEMA KWENDA CCM.
    UFUASI WA DINI SIYO SAWA NA UFUASI WA CHAMA CHA SIASA AU TIMU YA MPIRA, IT GOES DEEPER.

    ReplyDelete
  30. Akili yake haijadumaa. Mie pia ntamshangaa anayehama dini kama vile ninavyomshangaa aliyehama chama.
    unahama nyumba mtaa na shule, sio chama au dini kwa vile it concerns faith and commitment. Watu wanahama dini kama wamewapata wenzao wenye imani nyingine. Huamki tu na kusema imebadili dini, labda akili yake iwe imedumaa au ulienda ile dini kufuata maslahi fulani, na vile huyapati ndio unahama. Sawa sawa na Lowassa na huyu mwenzie, kuna wanachokitafuta chadema aidha kuwavuruga au maslahi yao maana sio bure la akili zao xiwe zimedumaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...