Wakazi wa Kata ya Kimbiji,Wilaya Temeke mkoani Dar-es-Salaam wamemchagua tena katikakura za maoni Diwani wao Mheshimiwa Muhidini Bunaya Sanya kugombea tena nafasi ya udiwani wa Kata hiyo ya Kimbiji hiliyopo wilaya Temeke.  Diwani wao huyo kijana Muhidini Bunaya Sanya (pichani) ameshinda kwa kura za maoni 1462 dhidi ya mpinzani wake ambaye alipata kura 68 tu,Kwa maana hii Kijana Muhidini Bunaya Sanyaamembwaga mpinzani wake kwa tofouti ya kura 1394 !
Mheshimiwa Muhidini Bunaya Sanya amefanikiwa tena kukitetea kiti chake cha udiwani wa kata ya Kimbiji kuelekea katika uchaguzi mkuu 2015  kwa kupitia tiketi ya chama cha CCM.
Diwani Muhidini Bunaya Sanya anajulikana sifa  za kuwa ni mchapa kazi,mbunifu na mpenda maendeleo mwenye uchungu na Kimbiji ambaye
katika kipindi kilichopita alisimama kidete ufanikishaji wa ujenzi wa shule za
Msingi na sekondari katika kata ya Kimbiji,Uchimbaji wa visima vya maji na
usambazaji wa umeme ambazo huduma zote hizo kwa sasa zipo kata ya Kimbiji
iliyopo wilayani Temeke,mkona Dar-es-Salaam.
Wakazi wa Kata ya Kimbiji wanawaomba wananchi wote kusimama bega kwa bega  Bwana  Muhidini Bunaya Sanya ili aweze kututumikia tena katika nafasi ya udiwani na kutuwakilisha katika baraza la madiwani la wilaya ya Temeke. Pendekezo la kata ya Kimbiji Muhidini Bunaya Sanya aka Jembe La Pini wa Chuma
Usikose kuungana na wanakimbiji at www.facebook.com/wanakijiji.kimbiji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...