KISAKALE CHA BIBI NYAMIHEMBE WA WAZARAMO NI CHIMBUKO LA UTANI WA
WAZARAMO NA WANYAMWEZI.
Benjamin Sawe-WHVUM
HADITHI moja ya ajabu inayosimuliwa na wazee wa
kizaramo ni ile ya Nyamihembe aliyolewa Unyamwezi,msimulizi mmoja alisema haikuwa
Hadithi ya kweli, nayo ni hii, ( Hii ni Tanzu ya Fasihi simulizi)
Mzee mmoja wa Kizaramo alikuwa na binti mzuri
aliyeitwa Nyamihembe, mtoto wa kiti cha kwanza,(Mtoto wa kiti ni mwana Nyang’iti, ni utambulisho wa Mila na Desturi za
baadhi ya Makabila ya Pwani, hutumika katika shuhuri zote za kimila za
kurithisha vijana katika kundi la utu uzima) Baada ya kuvunja
ungo akatokea Mnyamwezi mmoja akamposa, na kufunga pamvu(Harusi), kisha akapewa Bibi huyo akaishi naye.
Lakini Yule Mnyamwezi
baadae alipendelea kurudi kwao unyamwezi pamoja na mke yule, basi akataka
idhini kwa wazazi akakubaliwa,akaondoka Uzaramo na mkewe hadi kwao
Unyamwezini.
Walipokuwa kule wakajaaliwa watoto wengi wa kiume
na wakike, waliishi kule Unyamwezi kwa miaka mingi hadi wale watoto wakawa watu
wazima, wakaoa na kuolewa, wakazaa watoto kadha wa kadha waliokua wajukuu wa
Nyamihembe.
Lakini watoto na wajukuu wa
Nyamihembe hawakupata bahati ya kufika Uzaramo
tangu kuzaliwa kwao ila kila mara bibi Nyamihembe alikuwa akiwasimulia habari
za Uzaramo kama hadithi tu.
Nyamihembe aliishi kule hata akawa mzee (ajuza),
maana hata wale wajukuu walizaa kisha wakajukuu, akawa na virembwe kadha wa
kadha,wakati ule yule Mzazi mwezake Mnyamwezi Uzee ulimkithiri akafariki Dunia.
Fanani wa Hadithi ni Mwaruka Ramadhani (1965)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...