Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band maarufu kama
FFU ughaibuni ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki Alien juzi wikiendi walifanikiwa kuwadatisha washabiki wa muziki nchini Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga.
Bendi hiyo yenye makao yake nchini Ujerumani inayoongozwa na mwanamuziki mahiri Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja,imejizolea umaarufu wa kimataifa kwa kutumia mdundo wake wa "Bongo Dansi" uliochanganywa na rumba la kukata na shoka mdundo huo umefanikiwa kuwazoa na kuwadatisha akili washabiki wengi wa kimataifa.
Ngoma Africa Band kwa sasa wanatamba na single CD yao mpya 'La Mgambo"
yenye mbili za kumuaga Rais JK.
Unaweza kuwasikiliza at www.reverbnation.com/ngomaafricaband au uungana nao at www.facebook.com/ngomaafricaband
Gwaride limenoga Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga.
Mashabiki wa Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga.
Mambo ya Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga.
Ngoma Afrika band aka ffu-ughaibuni aka watoto wa mbwa viumbe wa ajabu Anunnaki naona maafande wakisukuma gwaride mbele kwa mbele
ReplyDelete