Asha Kigundula
BENDI ya muziki wa Dansi, FM Academia ‘Wazee wa Ngasuma’ Ijumaa
hii ya Agosti 21 watafanya sherehe ya kuazimisha miaka 18 tangu
kuanzishwa kwake itakayofanyika kwenye Ukumbi wa The Arcade
House, uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana Rais wa bendi hiyo, Nyoshi
El Sadaat, alisema kuwa maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea
vizuri.
Alisema kuwa siku hiyo itakuwa maalum kwa wapenzi wao kuanzia wa
miaka hiyo mpaka sasa maana wataburudisha kwa kuimba nyimbo
mbalimbali ambapo wataanzia saa 4 mpaka saa 9,usiku.
Alisema katika onesho hilo ambapo kampuni ya Mabibo Bear kupitia
kinywaji cha Windhoek, wameandaa burudani ya kutosha kwa kupiga
nyimbo za albamu zao 10 ambazo wamezitoa na kutamba.
Saadat alisema kuwa usiku huo maalum wamewaalika wanamuziki
wao mbalimbali ambao waliwahi kufanya kazi katika bendi yao na
kutoa hata nyimbo.
"Ni siku muhimu kwetu tokea mwaka 1997 hivyo wale wanamuziki
wote ambao walikuwepo Academia watakuwepo watapanda jukwaani
na kupiga nyimbo zetu zote zilizotamba.
Saadat alisema wapenzi wao watakaoingia mapema wukumbi
watapata zawadi maalum ambazo wameandaa pamoja na wadhamini
wao Windhoek.
Alisema kuwa hata hivyo katika usiku huo watatambulisha nyimbo zao
mbili ambazo ni Dada wewe pamoja na Moyo wangu.
“Niwatake wapenzi wa FM Academia kuhudhuria bila kukosa ndani ya
Arcade House, Mikocheni maana siku hiyo itakuwa moto,
tutatambulisha vibao viwili ambavyo ni Dada Huyo na Moyo Wangu.
Pia watakuwepo wakali waliowahi kupita kwenye bendi yetu akiwemo
Ndanda Kosovo, Jose Mara, Mkabeza na wengine kibao,” alisema
Nyoshi.
FM Academia ilianzishwa mwaka 1997 baada ya mmiliki wa mwanzo
kabisa wa bendi hiyo, Felician Mutta kufanya makubaliano ya
kuanzisha bendi na Nyoshi El Sadaat ‘Sauti ya Simba’ ambapo staa
huyo alishirikiana na watu wake waliokuwa wanaishi Kenya kwa kipindi
hicho.
FM Academia aliyekuwepo wakati FM Musica International ikizaliwa
mwaka 1997 ndani ya Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam.
Kwa sasa bendi hiyo inaundwa na vichwa hatari wakiwemo King
Blaise, Pablo Masai, Ben Byevanga, Jesus, Patcho Mwamba na
wengine wengi.
FM Academia iliyoanzishwa mwaka 1997 kwa jina la FM Musica
International, itatumia onyesho kutambulisha nyimbo zao mbili mpya
ukiwemo “Dada Wewe” utunzi wake King Blaise.
Albamu 10 ambazo toka ianzishwe bendi hiyo ni Atomic, Internet,
Prisons, Fredom, Mpambe nuski, Dotnata, Dunia Kigeugeu, Heshima
kwa wanawake Vuta nikuvute na Chuki ya nini.
Katika usiku huo kiingilio kitakuwa shilingi 10,000 kwa
kawaida na VIP itakuwa shilingi 20,000.
Mtupie Youtube sherehe hiyo ya miaka 18 ya FM Academia maana pia mna washabiki wengi tu ambao wanaishi ktk Diaspora na tukija nyumbani lazima tufike kusapoti wazee wa Ngwasuma.
ReplyDelete