Balozi
wa China nchini Tanzania Dr.Lu Youqing (katikati) akipata
maelekezo kuhusu bidhaa za Huawei wakati wa mkutano wa watanzania
waishio uhaibuni (Tanzania Diaspora).Kushoto ni Afisa mahusianao na
habari,Jimmy na kulia ni Meneja wa bidhaa na huduma wa Huawei hapa
nchini, Joseph
Lyimo Huawei walikua ni wazamini wakuu wa mkutano
huo ulifanyika jijini Dar es salaam katika hoteli ya Serena Augost 14
mwaka huu.
Dr.Lu
Youqing lieleza kuwa sasa hivi China na Tanzania wana
ushirikiano mzuri ambapo China imekuwa ikisaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania
kwa kuwawezesha watanzania waliopo nchini China.
Mbali na hayo wamekuwa wakisaidia Tanzania kwa njia nyingi moja wapo kwa makampuni ya nchi yao kuwekeza
nchini Tanzania.
Huawei ni moja ya kampuni hizo ambapo ina wafanyakazi wengi
watanzania na imekuwa ikisaidia watanzania katika mambo mengi ya kielimu na
kiteknolojia na kupelekea kukuza uchumi wa tanzania.
Huawei
Tanzania walikua moja ya wadhamini wa kongamano hili
la siku mbili ambapo kampuni ya Huawei walionyesha jinsi Kamera za CCTV
zinavyofanya kazi katika lango kuu la kuingilia katika kongamano hilo
ambapo kamera hizo zilionyesha vyema jinsi ya kumwona mtu ambaye anaweza
kufanya uharifu wowote mahali pale.
Pia
Huawei walikuwa na redio za 4G ambazo walikuwa wakizionyesha katika
mabanda kabla na baada ya wanatanzania waishio ughaibuni kuingia na
kutoka kujionea vifaa hivyo vinavyofanya kazi.
China imekua na ushirikiano mzuri na Tanzania na imetoa kipaumbele
kwakufadhili kongamano la wanaDiaspora nje ya nchi kwa kuwapatia elimu na vitu vingine.
Mbali
na Hapo China imewekeza mambo mbalimbali nchini Tanzania hasa katika Elimu na Teknologia.
Waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Bernad Membe amwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano uliowakutanisha watanzania waishio ughaibuni uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...