Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea mwenza
wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwasalimia baadhi ya Wanawake wanaounda
Baraza la Wanawake wa Chadema, waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya
Jengo la LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam, wakati walipowasili kwa
kuhutubia Baraza hilo.


Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza
machache wakati akiwasalimia maelfu ya Wanawake wanaounda Baraza la
BAWACHA, waliokuwa wamekaa nje ya jengo la LAPF kutokana na kukosa
nafasi ndani ya Ukumbi huo. Mh. Lowassa alilazimika kusimama na
kuwasalimia kinamama hao kabla ya kuingia Ukumbini kulihutubia Baraza
hilo.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimueleza jambo,
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA), Mh. Halima Mdee
wakati akilihutubia Baraza hilo.
KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA
KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA
Sura nyingi ni za kutoka kulekule sioni za pwani mbona mnalazimisha kwenda ikulu WHY? basi huo Ukakasi wenu oops sorry Ukawa wenu mngekuwa basi mnafanya na mambo ya kimaendeleo japo tuyaone machoni mwetu hakuna hata moja mnalolifanya zaidi ya KUANDAMANA JUU YA BARABARA ZA MAGUFULI ni mimi wenu muona mbali @team magufuli#hapakazitu watu gani msiokua na SHUKURANI nyie? mtapofuka macho mungu yupo Mjomba Michuzi sambaza upupu wangu ili wajikune
ReplyDeleteJamani leo Halima Mdee mnyenyekevu kweli kwa mtu aliyekuwa anadai ni fisadi namba moja!! Kweli hujafa hujaumbika!!!
ReplyDeleteYaani, Chadema tumechelewa kiasi kwa dada mdogo Halima Mdee kutukumbusha kuwa tumesahau akina mama?
ReplyDelete