Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza eneo hilo ili kujionea hali halishi ya biashara ndogo ndogo. Mh. Lowassa aliianza ziara yake eneo hilo la Gongo la Mboto na baadae alipanda daladala mpaka Pugu Kajiungeni, jijini Dar.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na vijana wanaoendesha Bodaboda waliokuwepo kando ya Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa ndani ya Daladala alilopanda kutokea Gongo la Mboto Mwisho mpaka Pugu Kajiungeni jijini Dar es salaam,mapema leo asubuhi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mtaka cha uvunguni hata kinyesi atalamba! .......Yeye ndo leo anapanda daladala?! Classic Lowassa at his best!

    Mwambieni Dr Magufuli mama yake alitembea kwa miguu kwenda kujifungua toto John Pombe Magufuli! Yani hata hela ya kupata da dala dala hakuwa nayo!

    Dr Magufuli amezaliwa kwenye dhiki za Tanzania, amekuli kwenye dhiki ya Tanzania, amesoma elimu yake mpaka PhD hapo hapo Tanzania kwasababu hakuwa na uwezo wala connection ya kwenda kusoma nje ya nchi kama Lowassa. Hivyo Dr Magufuli anaelewa umasikini na shida za Watanzania kuliko Lowassa kwani yeye mwenyewe alisha wahi kuwa masikini na bado baadhi ya ndugu zake pamoja ni masikini siyo kama huyo wa "chakawa" sijui Chadema ambaye anafanya maigizo oops! Nimekumbuka kuiga / Sanaa ndiyo fani aliyosomea hahahh!......#MagufuliNdiyoMpangoMzima , #HapaNiKaziTuu , #WanawakeTaifaKubwaMagufuliIkuluLazima
    #UtaisomaNumberMwakaHuu
    #IkuluSiyoMovieTheater



    Mwambieni Lowassa aache kutudhihaki siye wapanda dala dala!! #UnafikiMtupu #WiziMtupu

    ReplyDelete
  2. No no no no no and noooo nimuulize swali dogo tu mbona hukufanya HIVI? muda wako wote wa ujana wako na muda wote uliofanya kazi ndani ya SERIKALI mpaka Leo hii acha kabisa kutania watanzania uzee wote huo bado unautamani URAIS mimi ni Chadema lakini sasa 100% nnamashaka na wewe mzee wangu sorry kwa hilo mungu ibariki Tanzania yetu

    ReplyDelete
  3. MBOA HII NI BONGO MOVE ! inaeleweka kuwa Lowassa ni msanii

    ReplyDelete
  4. UNAJUA KUNA UHONGO MWINGINE HAUFANANI KABISA NA ANAYEONGOPA SASA KATIKA AKILI ZA KIKAWAIDA TU MAIGIZO HAYA MBONA AILETI MAANA WALA KUINGIA AKILINI ?

    ReplyDelete
  5. Mkuu mzee Lowassa huu mchezo wa kuigiza acha! usicheze na maisha yetu haya ya uswahilini tuachie wenyewe,sasa hapa ndio mnataka kutuambia nini? kuwa utakuwa unaenda Ikulu na dala dala?

    ReplyDelete
  6. Kwa kipindi hiki cha mbio za uchaguzi hatukushangai Lowassa kupanda dala dala au pengine kununu chakula kwa kina mama ntilie- sisi wenye tunajua wa kumpa kula wewe huna chako wenzie wote wamepumzika nawe ungana nao
    HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  7. Kampeni ziko za aina nyingi.

    ReplyDelete
  8. Usanii nao ni aje?

    ReplyDelete
  9. Hii mbona ipo staged?? Cameras kibao kwenye daladala, zimetoka wapi? Kweli shahada ya maigizo inafanya kazi.

    ReplyDelete
  10. hahahahaha...huyu jamaa sidhani kama amewahi kupata TAXI au DALALADA for the past 30 years.Sidhani kama watoto wake wanajua hata seat za daladala zikoje. USITUDHIHAKI, Umekula maisha muda wote huo gafla unataka kumake fun of our lives. Haya kapange basi chumba kimoja TANDALE KWA MTOGOLE uoge na kujisaidia choo cha nje ili ujue maisha yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...