Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiwapungia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa Chama hicho, wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni Jijini Dar es Salaam jioni ya leo. Mh. Lowassa alifika ofisini hapo kurudisha fomu za kuomba ridhaa ya Chama hicho, kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.Kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Mh. Godluck Ole Medeye alieambatana nae.
 Mkurugeni wa Oganaizesheni na Uratibu wa Kanda wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Benson Kigaila akionyesha fomu zenye idadi ya wananchi waliomdhani Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama hicho, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa. ambapo jumla ya wananchi 1,662,397 walijitokea katika maeneo mbali mbali kumdhamini Mgombea huyo.
 Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) akikabidhi fomu hizo kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof. Abdalaah Safari wakati wa hafla fupi ya kurudisha fomu hizo, iliyofanyika jioni ya leo kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni Jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Wadhamini wa CHADEMA, Mh. Arcado Ntagazwa na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Rais wa awamu ya TANO

    ReplyDelete
  2. Siku mbili zilizo pita, tarehe Agosti 30 Lowassa alichukua fomu ya kuwania urais. Leo tunaambiwa amekusanya zaidi ya wadhamini milioni 1.6! Sikatai hio idadi, ila waTanzania wa leo naamini hatukubali takwimu bila kupata ushahidi [evidence].

    Mi naomba nipendekeze, idadi hiyo ikaguliwe [audited], vinginevyo hauna thamani wowote kwangu mie. Yaani siku mbili tu amwezikusanya wapi? Au kanuni za Chadema si lazima mgombea aende mwenyewe kuomba udhamini mikoani?

    Lowassa ametumia haki yake ya kikatiba ya kutaka urais. Wasiwasi yangu ni kwa nini imemchukua zaidi ya miaka saba kutuambia yale yaliotokea mwaka wa Richmond? Leo mzee anakuja na anatuambia eti Katibu Kiongozi Philemon Luhanjo alikataa pendekezo lake? Kwa nini hakujiuzulu pale pale alipokataliwa na leo angeitwa msafi! Kwa nini alisubiri mpaka mapendekezo ya kamati isomwe?

    Sisi WaTanzania tuliounganishwa kwa gridi ya umeme ya kitaifa tuliteseka sana kwa kutopata umeme! Wagonjwa hospitalini, waliomiliki migahawa hawakuweza kuhifadhi vyakula kwenye friji, saluni, n.k. Je, tuliwahi kusikia umeme ikikatwa pale mahali patakatifu cha Ikulu au kwa nyumbani kwa Waziri Mkuu? Hata kama ilikatika [fluctuate] naamini walikuwa na standby genereta! Kwa hio ni sisi tulioteseka.

    Nimemsikiliza angalu mara mbili akiulizwa kuhusu utajiri wake. Amewataja ng'ombe zake 800 tu na alikwepa kujibu [dodge the question] kwa kusema hapendi umaskini. Naomba niulize, nani anapenda umaskini??? Kwa hiyo, atuambia chanzo.. na si kutokujibu. Kama leo anatukwepa, je akiwa rais hana budi kuyarudia tabia hilo la kutokujibu maswali. Na hao marafiki wake [friends of lowassa] pia waondoke rasmi.

    MTz.

    ReplyDelete
  3. Hao wadhamini watasubiri sana kulipwa pesa zao vyama vya upinzani wajipange sana kupata uraisi bado wabunge na madiwani watawapata sana Ila urasi bado ni shida, Magufuli ni mlalahoi na kura zake atazipata kupitia sisi walala hoi matajirina familia za wafanya biashara watampa lowasa sasa fikiria maskini wako wangapi? Lowasa bado atakua raisi wa Arusha na Kilimanjaro soi wa Tanzania.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tumi akili ww usifikirie na magoti unaleta mambo ya ukanda hii nchi ni yetu sote endelea kujifariji eti magufuli ni mlala hoi nyinyi ndio waliwao

      Delete
  4. Hilo nalo nenoo

    ReplyDelete
  5. Eti million moja na .....lo hatu danganyiki Mwarimu Nyerere alisha twambia muogopeni mtu anae taka kwenda ikulu kimabavu kama UKOMA sasa wewe uzee wote huo bado hata huoni aibu wala woga? hapa lazima kuna ajenda sio bule watanzania ndugu zangu lazima tujiulize huyu amekua serikalini kwa miaka mingapi? Na mala ngapi alishasema anauchukia UMASIKINI wakati yuko serikalini? jibu ni hapana yaani hajawahi kusema hata mara moja sasa why Leo hii anasema anauchukia UMASIKINI? chonde chonde watanzania wezangu tumpeni ushindi wa kishindo Dr MAGUFULI au jembe au tingatinga huyu ndio mtu pekee wa kuufuta UMASIKINI na Tanzania itakua nchi ya mfano ndani ya Africa ya Mashariki coz hakuna asiejua utendaji wake wa kazi Tanzania nzima so kwenye uteuzi wa mawaziri wake hakutakua na mawaziri MIZIGO wala wakuu wa mikoa na wakuu wa wiraya MIZIGO.

    ReplyDelete
  6. ASITUCHANGANYE SISI . HAO WALIOMPOKEQ WALITUMIA MIAKA NANE KUTUSOMESHA HUYO MZEE NI FISADI LEO HII WAMETUMIA DAKIKA TANO TU KUSEMA NI MSAFI NA MBWEMBWE NYINGI MPAKA MGOMBEA WA URAIDI .AKAJIPANGE UPYA .MFYUUUUUU

    ReplyDelete
  7. In short LOwassa Hafai! Hafai! Kama mheshimiwa anavyosema hapo chini labda awe raisi wa Arusha na Kilimanjaro but not kwa Tanzania......kwanza hatutaki MTU mwenye maamuzi magumu tunataka MTU mwenye maamuzi ya busara na ya msingi kwa faida ya waTanzania..maamuzi magumu hata majambazi wanafanya

    ReplyDelete


  8. JPM for President!!!

    Tumeona UTENDAJI wake, pia, in CHAGUO BORA kuliko WOTE!!!

    Natoa CHANGAMOTO KIFIKRA...ingetokea leo hii WaTZ tufanye kazi iliyofanywa na NEC na CC Dodoma...








    95% JPM angepita.................sooooooooo OBVIOUS!

    ReplyDelete
  9. MichongomaAugust 02, 2015



    -Naipenda nchi yangu TANZANIA

    -Naipenda TABIA ya WaTZ ya KUFUATILIA MAMBO KWA KARIBU

    -Nawakumbusha ndugu zangu WaTZ...




    Kuna issue huyu mokonzi aliishughulikia FROM HIS HOTEL SUITE somewhere ulaya....alisaini mkataba wa masilahi ya TAIFA, chumbani hoteli!...Richmond sijui...mazingira TATA...


    JK1 alishamgutukia...

    ReplyDelete
  10. Kizi mkazi,, ndugu yangu jinsi gani unavyoonekana ujui haki yako,mageuzi ni kwa njia nyingine ni mabadiliko,TANZANIA inahitaji mabadiliko,period.na hayo mabadiliko yataletwa na vyama vya upinzani,maana aiwezekani wewe ukaishi na chama kimoja kinakuongoza mpaka kinajisahau kwamba kuna wananchi walalahoi wanahitaji kuangaliwa,miaka karibia 54 linchi umeme hovyo,miundombinu hovyo,tunashindwa hata na ETHIOPIA,nchi miaka ya 70 mpaka 90 ilikuwa inajulikana kama nchi ya NJAA..leo hii ebu tembelea tuu ETHIOPIA ukaone,maajabu,unataka ccm halafu baadae unaanza kulalamika ohooo umeme,sijui,shule ghali,maisha magumu,..jifunza kitu kinahitwa mabadiliko,ndio maana mwanadamu anagundua kila leo vitu ,hiyo maana yake mabadiliko,toa hii unaweka hii,ukona haifai unaweka nyingine,sasa wewe na wenzako kaeni na ccm ..madadiliko ya nchi lazima wananchi waamue maamuzi magumu sana kuachana na chama ambcho kimekaa madarakani karibuni maisha yetu yote mpaka leo hi hakuna la maana,.na kiongozi bora ni yule mwenye maamuzi magumu,sio ya kucheka cheka,

    ReplyDelete
  11. Mdau unaetetea Ethiopia.. naomba nikuulize, je, unafahamu kuhusu haki za binadamu kama zinazingatiwa pale Ehtiopia? Obama juzi tu alipoitembelea, activists walipiga kelele! Pia, jiulize, wananchi wa Ethiopia wanakimbia nini kama hakuna njaa? Tunasoma kwenye vyombo vya habari ndugu zetu waEthiopia wakikamatwa na jeshi letu wanaposafiri kuelekea South Africa na wengine labda wanazama kwenye bahari la Mediterranean wakielekea Ulaya. Umewahi kusikia waTanzania eti wamo? Hata kama wapo, ni wachache sana.

    Afadhali sisi hapo tuna demokrasia [ingawa si bora sana] lakini ukilinganisha na nchi zingine za EAC, Tanzania inaongoza kwenye Freedom House Index! Usiwe mnafiki!

    ReplyDelete


  12. Kaka (au dada) Kizi Mkazi

    Njaa iko unyamwezini ndugu yangu, kuna njaa, idadi ya watu tena WENYEJI wa kule, wanaoishi kwa kutegemea misaada ya chakula CHA BURE, INAZIDI KUONGEZEKA SIKU HADI SIKU chakula kinacholengwa kwa 'wasiokuwa na makazi', kinawasitiri sio 'wasiokuwa na makazi' tu, ni WENYEJI, wafanyakazi wa kima cha wastani...nyamwezini kama unanielewa, Uingereza hakukaliki maisha magumu sana, njaa, idadi ya watoto wenye unyafuzi inaongezeka...Portugal, Italy, Greece, Spain...Njaa imezagaa ULAYA pia...

    Maajabu unayoyazungumzia Ethiopia ni yepi?

    Dunia NZIMA Ina njaa zama hizi. TOFAUTI ya WaAfrika ni kwamba wengi wetu tunazaliwa NDANI ya 'MITIKISIKO' bongo zetu "tunachacharika", ujanja, UPATU, kiubishiubishi tunasema, menzetu huko kwenye "maajabu", mtikisiko kidogo...uchizi


    Kipimo chako cha njaa kinavuja...wapi duniani HII LEO, hakuna "maisha magumu"?

    JPM akibaki na timu ambayo HAIJAKALIA KUMKOMOA kama walivyomfanyia JK, ili aonekane HAFAI. Mabadiliko tutayaona. Tingatinga yani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...