Na  Bashir  Yakub.
Kumekuwepo  na  sintofahamu   nyingi  kwa  madereva  na  watumiaji  wengine  wa  vyombo  vya  usafiri. Sintofahamu  hii  imekuwa  ikiletwa  na   baadhi  ya  mambo  ambayo  hayaeleweki  sawasawa  katika  suala  zima  la  usalama  barabarani   na  sheria  zake. Wadau   wa  barabarani wamekuwa  wakilaumiana,  madereva  wakiwalaumu  askari  wa  barabarani  kwa  uonevu  huku  askari  wa  barabarani  wakiwalaumu  madereva  kwa  ukorofi   na  ukosefu  wa  utii  wa sheria  bila  shuruti. Lakini  swali  hapa  ni  kwanini  iwepo  mivutano  na  hali  kuna  sheria. Sheria  inasemaje  kwa  kila  jambo  ambalo  wadau  hawa  wanatofautiana?. 

1.UBABE  WA  ASKARI  WA  BARABARANI.

Baadhi  ya  askari  wa  barabarani  wamekuwa  ni  wababe  sana. Wanahoji  mambo  ambayo   si  wajibu  wao  kuyahoji  na  hawataki  dereva  aulize  lolote  kuhusu  kuhoji  kwao  mambo  hayo. Wanataka  kila  wanachosema  dereva atii  hata  kama anaona  hakipo  kwa  mujibu  wa  sheria. Matokeo  yake  mtu  anaandikiwa  faini  za  makosa  mengi  ilimradi  tu  kumkomoa. Askari wengine  wamefikia  hatua  ya  kuwapiga madereva  vibao.  Binafsi  nimewahi  kushuhudia  askari  wa  usalama  barabarani  akimnasa  kibao  dereva wa  daladala. Ni  ubabe  uliovuka  mipaka  na  hakika  ni  uvunjaji  wa  sheria  uliopitiliza .

2.  JE  TRAFIKI  ANARUHUSIWA  KUMNYANGANYA  DEREVA  LESENI.

Masuala ya usalama  barabarani   yanaainishwa  ndani  ya  Sheria  ya  Usalama barabarani ( The  Road  Traffic Act) ambayo  ndio  hueleza  wajibu   na  haki  za  kila  mdau  na  mtumiaji  wa  barabara. Katika  sheria  hii  hakuna  pahala pameandikwa  kuwa  trafiki  achukue  leseni  ya  dereva  kwa  kuwa  dereva  ametenda  kosa   fulani. Maana  fupi  ya hili  ni  kuwa  trafiki  haruhusiwi  kuchukua  leseni  ya  dereva.  Anachoweza kufanya  trafiki  ni  kile  kilichoainishwa  na  kifungu  cha  17  cha  sheria hiyo  ya  usalama  barabarani. Kifungu  hicho  kinampa  trafiki  mamlaka  ya  kukagua  na kujiridhisha   na  uhalali  wa  leseni  ya  dereva. Hakisemi  aichukue. Kinasema  aikague  basi.  Kukagua  na  kuchukua  ni  mambo  mawili  tofauti.  

Kama  hivyo  ndivyo  basi  yafaa  kueleweka  kuwa   kitendo  cha  askari  kumsimamisha  dereva  na  kisha  kumpokonya  leseni  yake  ni  kinyume  cha  sheria.  Dereva  anao  wajibu  wa  kulinda   haki  hii  kwa  kulikataa  hili na kuhakikisha trafiki  hamfanyii  kitendo  hiki.  Kumbuka  kuwa  wakati  askari  wa barabarani  akitekeleza  wajibu  wake  wa kisheria  na  wewe  dereva  unayo  haki  ya  kutetea  haki  zako  za  kisheria. Hakuna  aliye  juu  ya  mwingine kwani  anatekeleza  wajibu  nawe  unalinda  haki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hii ni kweli kabisa...traffic polisi wanaharibu jina la tz..mimi pia waliwahi kunikamata bila kosa..baada ya kumuuliza yeye ni nani akasema swali gani hilo huoni kama nimevaa uniform..nikamwambia naona umevaa nguo nyeupe lakini sioni namba zako za kazi akaja juu namba utaziona kwenye karatasi za kwenye sharti nitakuwa nimedondosha...nikamwambia za kuandika kwenye karatasi hata mimi naweza kuandika....kwahiyo utani dhibitishaje kama wewe ni trafic polisi akawa mbogo nikamwambia usinifokee mi sio mwanao...wakaja na wenzake wengine wakanaza kuniambia wewe dada mkorofi nikawauliza kuuliza namba za polisi ndio ukorofi mwanamke trafic akanijibu utamuulizaje polisi...nikamwambia zamani wakati tulikuwa gizani ndio yulikuwa hatuuulizi ...wacha wafoke wote twende kituoni...nikwaambia twendeni mara eti wapande gari langu nikawaambia hakuna nafasi nikasumbuana nao sana hatimaye tukaenda kituoni...kufika huko boss hayupo jamaa tuliemkuta hapo kalewa balaa na uniform zake mbona majanga tunasafari ndefu sana ya kuelimishana...hilo halikunipa tabu mimi niliona ni challenge nzuri sana sikunyingine hata onea watu ....lakini wazungu wageni wanapata tabu saaana na hao trafic kiasi kwamba wakirudi makwao wanaweka kwenye holiday review zao na jina la tz linaharibika kwa sababu ya wachache wasio thamini kazi zao na nchi yao wanaangalia maslahi yao tu...hawa polisI wanatakiwa kuelimishwa na kufahamishwa umuhimu wa watalii ktk nchi yao..sio wanaona ni wazungu basi wanawaona wajinga au hawajui kitu hao au hawajui kiswahili wanatumia nafasi hiyo kuharibu jina la tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...