Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua
Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za Sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa
Binadamu, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo Agosti 21, 2015
kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa
ya kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Kinemo Kihonamo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za Sheria ya kuzuia
usafirishaji haramu wa Binadamu, uliyofanyika leo Agosti 21, 2015 kwenye
Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni
rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
Baadhi
ya Wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni
rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakijisomea vipeperushi
walivyogaiwa katika uzinduzi huo.
11 hadi 16:-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya viongozi na wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo, baada ya uzinduzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...