Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi
Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Erasmus Rugarabamu kwa niaba ya
Menejimenti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa akitoa pongezi kwa Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Mkoa
wa Ruvuma kwa ushindi mnono alioupata katika kura za maoni za Chama cha
Mapinduzi (CCM) katika kutafuta mgombea wa ubunge Jimbo la Mbinga
Magharibi. Eng. Manyanya alishinda kwa kura 13,276 ambapo mshindi wa
pili alikua na kura 3,466. Jumla ya wagombea walikua 10 ambapo tisa kati
yao walikuwa ni wanaume.
Awali
Jimbo hilo lilikuwa nimeshikiliwa na hayati Capt. John Komba. Kwasasa
imebaki hatua ya mwisho ya majina ya wagombea kupitishwa na Uongozi wa
juu wa Chama kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi
majimboni katika uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu 2015. Uongozi na
Watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa unamtakia kila la heri
Eng. Manyanya katika safari yake hiyo na hatimae aweze kushinda katika
Jimbo hilo.
Akitoa
shukurani kwa niaba ya watumishi Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha
Serikali za Mitaa Ndugu Albinus Mgonya alimpongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa
Rukwa kwa msukumo mkubwa wa maendeleo aliouweka katika kipindi cha
uongozi wake hususani katika sekta ya elimu ambapo alianzisha Azimio la
Kasense kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu mashuleni, Kuboresha
afya ya mama wajawazito na watoto wachanga, usafi wa mazingira ambapo
alianzisha kampeni ya Sumbawanga Ng'ara iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa
Rais, Kampeni ya upandaji miti, kuboresha mazingira ya utalii katika
maporomoko ya Mto Kalambo, kuboresha hali ya ulinzi na usalama katika
Mkoa, Kuwaunganisha watumishi na viongozi katika kufanya kazi kwa
pamoja n.k
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
THIS IS THE REASON FOR ANY MWENYE UFAHAMU KUJIULIZA KAMA KWELI HAWA MA RC WANAHITAJIKA KWENYE MFUMO WETU WA MAENDELEO YA MIKOA. JUST A THOUGHT UNCLE MICHUZI
ReplyDelete