MIKOA 10 ya Tanzania bara, Inatarajia kuombea amani na utulivu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu hapa nchini.
Kwa mujibu  wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama mikoa hiyo itaiombea amani Tanzania kupitia muziki wa Injili kupitia waimbaji mbalimbali  wa ndani na nje ya nchi.

Msama alisema awali kabla ya mikoa hiyo kuombea amani uchaguzi Mkuu, Tamasha la kwanza lenye dhamira hiyo litafanyika Oktoba 4 jijini Dar es Salaam.

“Tumeona kuna umuhimu kuwashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kumuomba Mungu atuongoze katika uchaguzi Mkuu ambao unatakiwa kuwa huru na haki, ili kufanikisha hayo kwa ufanisi nyimbo za kumuomba na kumtukuza Mungu zitumike ili dua na sala zisikike mbinguni,” alisema Msama.

Msama alisema Kamati yake bado inaendelea na mchakato wa kufanikisha maandalizi ya tamasha hilo ambalo litaimarisha na kudumisha amani na utulivu ulioasisiwa na baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere.

Aidha Msama alisema tamasha hilo litashirikisha waimbaji mbalimbali wakiwemo wa Tanzania na nje  ambao watasaidia kufikisha ujumbe huo kwa Mungu.


Msama alisema wananchi wajiandae kupata neno la Mungu kupitia waimbaji wa nyimbo za Injili ambao watafanikisha mungu kusikia wanachohitaji wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. GOT ONE WORD FOR YOU "OPPORTUNIST"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...