Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru (Mwenye miwani) kuzungumza na wafanyakazi alipotembelea bodi hiyo jana.
Mmoja wa wafanyakazi wa TTB Bw. Geofrey Tengeneza ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano akielezea jambo kwa Katibu Mkuu alipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania na kuzungumza na wafanyakazi.  
 Baadhi ya wanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania wakimsikiliza kwa makini  Katibu Mkuu Dk Meru alipokuwa akizungumza nao.

 Na: Geofrey Tengeneza
Wizara ya Maliasili na Utalii imeahidi kuupa kipaumbele mchakato wa kuifanya Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) kuwa Mamlaka ya Utalii Tanzania (TTA) kwa lengo la kuiwezesha Bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kutekeleza majukumu yake kikamilifu. Aidha Wizara hiyo imeitaka TTB  kuangalia ni maeneo gani yanaweza kuwa ni vyanzo vya mapato vitakavyoiwezesha Bodi kujiingizia fedha.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru  alipotembelea Makao makuu ya Bodi ya Utalii yaliyoko katika jengo la IPS jijini Dar es salaam na kuzungumza na wafanyakazi wa bodi hiyo.
Dkt Meru ameipongeza   Bodi ya Utalii kwa kuendelea kufanya kazi vizuri katika mazingira yenye changamoto nyingi hasa za kifedha zinazoikabili. Amesema TTB ndiyo chombo chenye dhamana ya kutangaza vivutio vya utalii kwa ujumla wake, hivyo kinapaswa kuwezeshwa kutimiza jukumu hilo kwa niaba ya nchi badala ya kila taasisi kutangaza vivutio inavyosimamia.
“Tunawajibu wa kuwawezesha TTB mtekeleze majukumu yenu vizuri kwa kuwa ninyi ndio hasa mliokabidhiwa jukumu la kutangaza vivutio vyetu vyote vya utalii kama vile vya kihistoria, fukwe, wanyama, milima na kadhalika” alisema.


Hii ni ziara ya kwanza ya Dk Meru kutembelea Makao Makuu ya ofisi za Bodi tangu kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo. Bodi ya Utalii Tanzania ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara yake yenye jukumu la kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...