MKURUGENZI wa Shirika Hifadhi ya Jamii  (NSSF), Ramadhan Dau amewataka  madereva na wamiliki wa pikipiki za Bodaboda kuwa na utamaduni wa kurudisha mikopo wanayopata kupitia Zao ili iweze kuzungushwa kwa bodaboda wengine.

Dau ametoa rai hiyo leo wakati alipokuwa akitia saini hati ya makubaliano ya ushirikiano kati NSSF na  Baraza la Taifa  la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC).

“Hamkufanya makosa kujiunga Saccos, kwa kuwa nina imani mtapata nafasi ya kukopeshwa na mtapata maendeleo, hivyo ni matarajio yangu kuona kwamba yule bodaboda aliyepata mkopo siku moja nije kusikia anamiliki ndege,” alisema Dau.

Makubaliano hayo ya mkopo wenye thamani ya Shilingi bilioni moja yalitiwa saini na Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa, huku akishuhudiwa na  wanachama wa Chama Cha Ushirika wa Akiba  na Mikopo Cha Wendesha Bodaboda Jijini Dar es Salaam.

Mkataba huo uliotiwa saini jana una lengo la kuisaidia serikali kutimiza wajibu wake kwa kuwasaidia vijana kutambua fursa na nafasi yao katika maendeo ya taifa, kama sehemu ya jitihada  za kuchangia  katika  kukabiliana  na tatizo la kuzalisha mali  kwa ajili ua ujenzi wa uchumi.

“Mkataba tunao saini leo ni moja  ya jitihada za kuchangia katika kukabiliana na tatizo hili. Kuanzishwa kwa programu hii kutasaidia vijana katika sekta hii ndogo ya usafirishaji kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kununua pikipiki zao wenyewe, kuanzisha au kuendeleza biashara nyingine na pia kupata huduma za matibabu na huduma nyingine zilizotolewa na NSSF,” alisema.

Fedha za  dhamana kwa ajili ya programu hiyo zitawekwa katika Benki ya Posta na NSSF itatumia  fedha zake kukopesha vijana kwa ajili ya kununulia pikipiki kwa lengo  la kufikia hesabu walizokubaliana na waajiri wao, matokeo yake kusababisha ajali mara kwa mara.

Akiweka wazi sifa na mashari ya wanachama ambao wataweza kukopesha ni wale ambao  watakuwa wako kwenye vyama kuweka na kukopa, Saccos ambavyo vimesajiliwa kisheria.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (kulia) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi Issa (kushoto) wakitia saini hati ya mkataba wa utekelezaji wa program ya NSSF Boda Boda katika hafla iliyofanyika mchana wa leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa NSSF Water Front, Jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto), ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Uwezeshaji wa NEEC, Edwin Chrisant, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Omari Issah, Mwenyekiti wa Dar es Salaam Bodaboda Saccos (DABOSA), Saidy Kagomba na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crecentius Magori.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi Issa (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau wakibadilishana hati baada ya kutiliana saini mkataba wa utekelezaji wa programu ya NSSF Boda Boda katika hafla iliyofanyika mchana wa leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa NSSF Water Front, Jijini Dar es salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Omari Issah.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...