Mgombea Urais wa Chama Cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe akipokea fomu ya kugombea urais kutoka kwa Afisa Mwandamizi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Adam Nyando katika ofisi za NEC leo jijini Dar es Salaam.
Mgombea Urais wa Chama Cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuchukua fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CHAUMA nje ya ofisi NEC leo jijini Dar es Salaam. (Pichana Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)



Na Chalila Kibuda, Globuya Jamii.
 MWENYEKITI wa Chama cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe amechukua fomu ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hizo Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), leo jijini Dar es Salaam, Rungwe amesema watanzania kama wanahitaji maendeleo wachague chama hicho na sio kuchagua watu wanaotaka kutumikia matumbo yao. Amesema zoezi la kuchukua fomu za urais ziko wazi na kutufanya wagombea kuwa huru katika zoezi zima kutoka na maandalizi yalifanywa na tume ys Taifs ys Uchaguzi.

Rungwe amesema mwaka 2015 aligombea kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi lakini kura hazikutosha na kufanikiwa kupata wabunge wawili kwa tiketi kwa chama hicho. Amesema ana uwezo wa kuwatumikia watanzania na sio kwenda Ikulu kwa ajili ya kutafuta jinsi ya kujinufaisha na kuwaacha watu walionipa ridhaa ya kuwaletea maendeleo.

Aidha amesema nafasi ya urais sio ya mchezo kutoka na na kuwa majukumu makubwa ya kuwatumikia watu katika kuwapa maendeleo yatayotokana nafasi hiyo.

 “Nina imani watanzania wataichaugua CHAUMA katika kuperusha bendera katika kuweza kupata maendeleo kama kauli mbiu ya chama kutaka ukombozi” anasema Rungwe. Vyama vilivyochukua fomu ya urais vimefikia vinnea mbavyo ni, Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), UPDP, Chama cha Democratic Party (DP), pamoja na Chauma.

Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli anatarajia kuchukua fomu kesho katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jijini Dar es Salaam. mwisho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...