Na Lilian Lundo, MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete  (Pichani)amezipongeza sekta binafsi kwa kukubali kusaini hati  ya ahadi ya uadilifu  katika harakati za mapambano dhidi ya rushwa na utovu wa nidhamu.

 Rais alisema hayo katika wakati akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa hati hizo zinazojumuisha sekta ya Umma na  Binafsi katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Katika hafla hiyo,  Mhe. Rais alisaini hati tatu ambazo ni Hati ya ahadi ya uadilifu ya Viongozi wa Umma, hati ya ahadi ya uadilifu ya Utumishi wa Umma na hati ya uadilifu ya Sekta Binafsi. 

“Ushiriki wa sekta binafsi katika hati hii utasaidia kuleta mabadiliko ya kuwa na mwenendo wa kimaadili ya mapambano dhidi ya rushwa” alisema Mhe. Kikwete.

Rais Kikwete alisema kuwa badala ya wananchi na sekta binafsi kulalamika pembeni ni vyema kuwasilisha malalamiko yao katika sehemu husika ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

 Aidha, Rais aliongeza kuwa baadhi ya sekta binafsi  zimekuwa zikiombwa na kutoa rushwa ili kupewa  upendeleo wa kupata  tenda serikalini, hivyo kwa kusaini hati   hiyo ya ahadi ya uadilifu kutaondoa mianya ya  upokeaji na utoaji rushwa katika sekta hiyo.

Hati ya ahadi ya uadilifu inakumbusha Makampuni, Viongozi na Watumishi wa Umma juu ya wajibu wao wa kuzingatia kanuni za maadili na mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Wazo la kuwa na ahadi ya uadilifu liliibuliwa katika maabara ya Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambapo ilionekanakuwa rushwa bado ni tatizo katika uendeshaji wa shughuli za Umma na Binafsi hususani utoaji huduma kwa umma na biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...