Spika wa Bunge Mhe. Anne
Makinda (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mhe. Clara Diana Mwatuka (Mb), aliyekuwa Mbunge wa Viti
Maalum, kupitia Chama cha Wananchi, (CUF) Mkoa wa Mtwara, kilichotokea jana Jumapili tarehe 9 Agosti 2015 kwa ajali
ya gari katika Kijiji cha Miyuyu, Newala, Mkoani Mtwara.
Mipango ya Mazishi inaendelea kufanywa na Ofisi ya Bunge kwa
kushirikiana na familia ya Marehemu, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika
kesho siku ya Jumanne tarehe 11 Agosti, 2014 saa 9:00 Alasiri, kijijini kwake Nanganga, Wilayani MASASI, Mkoa wa MTWARA. Taarifa
zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kadri zitakavyopatikana.
MUNGU AIWEKE
ROHO YA MAREHEMU
MAHALI PEMA PEPONI - AMINA!
MAHALI PEMA PEPONI - AMINA!
Imetolewa na:
Idara
ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi
ya Bunge
DAR ES SALAAM
10 Agosti, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...