WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL), Arusha juzi wameungana
na familia zao katika tamasha la familia( Family
Day),zilizofanyika katika viwanja vya TGT, vilivyopo eneo la
Kisongo,nje kidogo ya Arusha.
Aidha katika tamasha hilo wafanyakazi hao na familia zao walipata
fursa ya kushiriki michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa
miguu,kuvuta kamba,mpira wa mezani,kucheza muziki pamoja na michezo
mbalimbali ya watoto.
Kwa mujibu wa Mratibu wa tamasha hilo Optaty Minja,alisema kuwa
lengo la tamasha hilo ni kuonyesha jinsi kampuni hiyo ya bia
inavyothamini familia za wafanyakazi wake.
Minja ambaye pia ni Mhasibu wa TBL katika upande wa mashamba,alisema
kuwa kuwakutanisha wafanyakazi hao na familia zao kunawasaidia kuweza
kufahamiana , na kusaidia kujenga mahusiano mazuri baina ya familia
zao,kwani mara nyingi hukutana wakiwa kazini lakini watoto, wake na
waume zao hawafahamiani hivyo kupitia siku ya familia husaidia kujenga
uhusiano na kufanya kuwa familia moja.
“Kama kampuni tumeona ni jambo zuri familia zetu kukutana leo ili
kuonyesha jinsi gani kampuni inathamini familia za wafanyakazi wake
ambapo pia tunazidi kufahamiana,kujenga mahusiano mazuri kati yetu na
familia zetu kwa ujumla”alisema Minja
Baadhi ya familia za wafanyakazi wa TBL Arusha, wakipata chakula cha mchana katika viwanja vya
TGT,vilivyopo eneo la Kisongo,nje kidogo ya Jiji la Arusha,juzi katika
sherehe ya familia (family day) ya kampuni hiyo.
Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya TBL mkoa wa Arusha, wakipewa zawadi baada ya kushinda katika
michezo mbalimbali iliyofanyika katika sherehe ya familia (family day)
ya wafanyakazi wa kampuni hiyo,juzi,jijini
Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...