Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na kampuni za Maurel and Prom na Wentworth Resources, leo hii wameendelea na zoezi nyeti la kutoa gesi asilia katika kisima namba 3 kilichopo Mnazi Bay (MB3) kwenda katika kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo Madimba, Mtwara. 

Zoezi hili ni muendelezo wa ukamilishaji wa mradi mkubwa wa Serikali wa kuzalisha gesi asilia kwa madhumuni ya kuzalisha umeme hapa nchini.

Akiongea wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alisema “ ni furaha kubwa leo kuanza kuzalisha gesi asilia ya Mnazi Bay ambayo itaenda kuchakatwa katika mitambo yetu iliyopo Madimba na kisha kusafirishwa hadi Kinyerezi, Dar es Salaam ambapo wenzetu wa Tanesco wataitumia kuzalisha umeme”. 

 Dkt. Mataragio aliongeza kuwa kisima namba 3 (MB3) kina uwezo wa kuzalisha gesi asilia takribani futi za ujazo milioni 20 hadi 30 kwa siku (20-30mmscfd). Visima vingine vitakavyounganishwa ni pamoja na MX1, MB2, MB4 na MB1 hapo baadae na kufanya uzalishaji kufikia futi za ujazo milioni 130 kwa siku (130mmscfd).

Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Taifa la Mafuta (TPDC) limetekeleza mradi huu wa kipekee kwa madhumuni ya kukabiliana na tatizo la upungufu wa umeme hapa nchini. Hata hivyo, gesi asilia pia inatarajiwa kutumika viwandani kama nishati na pia malighafi, majumbani kupikia na katika magari. 

Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki kuwa na miundombinu mikubwa ya kusafisha na kusafirisha gesi asilia na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuuza gesi hata kwa nchi majirani hapo baadae.
Kisima namba 3 au MB 3 kama kijulikanavyo kimeanza kuzalisha gesi asilia leo hii ikiwa ni mojawapo ya visima ambavyo vitapeleka gesi asilia katika mitambo ya kuchakata gesi iliyopo Madimba. Mtwara.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (aliyeshika valvu) akifungulia gesi ya kwanza katika kisima namba 3 au MB 3 kama kijulikanavyo kuruhusu gesi kuanza kupita kuelekea katika mitambo ya kuichakata iliyopo Madimba, Mtwara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hatua ya kumalizika kwa matatizo ya umeme ni hatua nzuri kama tumeifikia sasa.

    ReplyDelete
  2. Hii ni hatua muhimu sana katika ustawi wa uchumi wa Nchi yetu Tanzania. Huu mradi kama utaendesha kwa uzalendo, kuna uwezekana mkubwa maisha ya kila mtanzania kwa moja kwa moja au kwa namna nyingine yakainuka. Watanzania tuna kila sababu ya kijivunia hatua hiituliyofikia leo. Hongera TPDC kwa kufikia hatua hii, na Dr. Mataragio kwa kuibeba dhamana hii.

    ReplyDelete
  3. Lakini matumizi ya makaa, gesi asilia na mafuta yanapigwa vita sana kwa kuchangia machafuko ya mazingira! Ni nyanzo nya nishati iiyopitwa na wakati - vya Enzi za Mapinduzi ya Viwndani. Sisi tukae kimya tu na kupuuza kauli zao; vinatusaidia kuendelea, ama sivyo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...