Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akimkabidhi kijana Prisca George Chilumba, msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Ligula, Manispaa ya Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu (wa pili kushoto) na rafiki wa Prisca.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akimkabidhi kijana Prisca George Chilumba, msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Ligula, Manispaa ya Mtwara jana. Anayeshuhudia (katikati) ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akifafanua jambo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, kwa kijana Prisca George Chilumba (kulia), katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Ligula, Manispaa ya Mtwara jana. Anayeshuhudia ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa
Bayumi (wa pili kulia), akimpongeza kijana Prisca George Chilumba, baada
ya kumkabidhi msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake
kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi
iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel
katika Mtaa wa Ligula, Manispaa ya Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni
wafanyakazi wa Airtel.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa
imemuwezesha mjasiriamali Prisca George Chillumba ambaye ni mmiliki wa
biashara ya saluni mkoani Mtwara. Prisca amenufaika na mradi huu kwa
kupatiwa vitendeakazi mbalimbali vitakavyomuwezezesha kupanua wigo wa
idadi ya huduma zitatakopatikana katika saluni yake.
Akikabidhi
vifaa hivyo meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi
amesema, sambamba na kuongeza idadi ya huduma zitakazopatikana katika
saluni ya Prisca, vifaa hivi vitamuwezesha kuhudumia wateja wengi Zaidi
kwa wakati mmoja, jambo ambalo litamuwezesha Prisca kuajiri vijana
wenzie ili kuendeleza biashara na kukuza kipato chake.
Bi
Bayumi amesema, mpango huo wa kuwawezesha wajasiriamali unawapatia
vitendeakazi vijana wajasiriamali ili kuwaongezea kasi ya maendeleo ya
kibiashara vijana hawa ambao tayari wameshachukua hatua na kuanza
kujishughulisha na biashara ndogondogo.
Lengo likiwa ni kurudisha sehemu
ya mapato yake kwa jamii katika njia inayoleta tija.
“Sisi
kama Kampuni ya mawasiliano tumeona ni vizuri kushirikiana na
wajasiriamali na hasa vijana ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza
mitaji yao ya biashara kwa mafunzo na vifaa” alisema meneja huyo.
Awali
akipokea msaada huo Bi Prisca ameshukuru kwa vifaa hivyo na kuahidi
kuendeleza zaidi biashara hiyo ili kutimiza ndoto zake za kuwa
mfanyabiashara mkubwa.
“Siamini kama naweza kufikia malengo
yangu katika biashra hii, naahidi kuongeza juhudi na kutumia vyema
msaada huu ili kuhakikisha nakuza na kuendeleza biashara yangu lakini
pia nitatoa fursa kwa viajana wenzangu” Alisema Priscar.
Kampuni
ya simu ya Airtel inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la
kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana ili
waweze kukuza mitaji yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...