Naibu waziri wa maji Amos G Makalla amefanya ziara ya kikazi wilaya ya Sengerema kwa kukagua ujenzi wa mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika na serikali ya Tanzania.
 Mradi huu unagharimu shilingi bilioni 20 na utanufaisha watu wapatao 108,000 hadi kufikia mwaka 2025 
Naibu Waziri wa maji ametembelea chanzo cha maji ziwa victoria kijiji cha Nyamazugo, ujenzi wa matanki maeneo ya Mwabaluhi na Igogo na kuwataka wakandarasi kampuni ya Kichina Ya CCECC ltd na mhandisi mshauri kampuni ya COWI kuongeza kasi ya ujenzi na kukamilisha ujenzi wa mradi ifikapo Februari 2016.
 Aidha ameagiza mkandarasi kuanza ulazaji wa mabomba kutoka tanki la Nyamazugo kwenda tanki la Igogo ili kuharakisha upatikanaji wa maji.
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano wakati mradi huu unatekelezwa kwani kukamilika kwa mradi huo kutawanufaisha wao wananchi wa sengerema Amepongeza jitihada za mkuu wa wilaya ya sengerema na mamlaka ya Maji mkoa wa Mwanza kwa pamoja wamewezesha mradi kufikia hatua nzuri
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Amos Makalla akiongea na waandishi habari eneo la Igogo
Mhe Makalla akiwa na  mhandisi mshauri wa kampuni ya COWI Bw. Michael Nyagabona


Mhe Makalla akikagua mradi huo

Mhe Makalla akiongea na Mkuu wa wilaya Sengerema bi Zainabu Taleck na wataalamu wa mradi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...