Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akihojiwa na Joseph Msami wa Radio ya Umoja wa Mataifa.
(Picha:UN-Idhaa ya Kiswahili/Assumpta Massoi)
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema wanawake hawajengewi mazingira ya kutosha ya ustawi wa kijamii na kiuchumi kama ilivyo wanaume hususani katika nchi zinazoendelea akitolea mfano wa bajeti za serikali ambazo hazizingatii ukuaji nwa kundi hilo.
Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii muda mfupi baada ya kuhutubia mjadala kuhusu kupambana na ukosefu wa usawa na kuwezesha wanawake na wasichana ikiwa ni sehemu ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs, Rais Kikwete anataja mambo kadhaa ambayo ni muhimu kwa wanawake ikiwamo elimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...