SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam
(DAWASCO), imezindua rasmi mfuko wa akiba na mikopo (Saccos) kwaajili ya
wafanyakazi wa shirika hilo katika harakati za kujikomboa kiuchumi na
kuimarisha umoja miongoni mwao.
Akiongea na wafanyakazi katika uzinduzi huo, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja amewahimiza wafanyakazi
kuitumia Saccos hiyo kujikomboa kiuchumi na kuondokana na utozwaji mkubwa wa
riba kutoka kwa baadhi ya taasisi za fedha, hali inayowaumiza watumishi wengi
nchini.
Uanzishwaji wa mfuko huo umelenga kuwasaidia
wafanyakazi kutatua matatizo ya haraka yanayojitokeza ndani na nje ya maisha ya
kazi na kuiweka Saccos hiyo kama sehemu ya Dawasco kujipanua zaidi katika
kujali maslai ya wafanyakazi wake.
Saccos ya Dawasco imezinduliwa ikiwa na mtaji wa
kuanzia wa Tsh Milioni 95 na jumla ya
wanachama736 huku Ndugu Ramadhani
Mtindasi akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Saccos hiyo na nafasi ya Makamu
Mwenyekiti ikienda kwa Erasto Emmanuel.
Mara baada ya uchaguzi huo, viongozi hao wamehaidi
kuleta mapinduzi na mabadiliko ya uendeshaji wa mfuko huo kwa kuhakikisha
unatoa unafuu kwa kila mwanachama na kuweka masharti rafiki ili kutimiza
malengo ya kuanzishwa kwake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...