Uongozi wa Africa Media Group Ltd kupitia Radio ya Magic Fm unasikitishwa kutangaza kifo cha aliyekuwa mfanyakazi mwenzao upande wa Radio,Geophrey Herry (pichani enzi za uhai wake), al-maarufu kama Dj Nature, kilichotokea siku ya Jumatatu ya tarehe 31/08/2015 mjini Songea.
Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki
na majirani popote pale walipo.
Mazishi yatafanyika kesho Songea.
Magic Fm inasikitika sana kwa kupotelewa na jembe,
lakini hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo.
Mungu ametoa, na Mungu ametwaa.
jina la Bwana na lihimidiwe.
Amen.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...