KATIKA kuhakikisha kuwa inamshirikisha msikilizaji wake kwenye kila jambo na hatua inayopiga 93.7 efm, kupitia kipindi chake kipya cha Uhondo ambacho huruka hewani kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa sita mchana hadi saa tisa Alasiri, Kikiwa na watangazaji mahiri Dina Marios na Swebe Santana (Rais wa Wanaume) kimeandaa shindano la Kanga kwa ajili ya wanawake wote wasikilizaji wa Efm 93.7
Lengo la shindano hilo, linaloanza leo Septemba 14 na kuishia Oktoba 5 mwaka huu, kwanza ni kuwahamasisha wanawake wote wakione Kipindi cha Uhondo kuwa kimekuja kwa ajili yao, pili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini pia tatu kumwonyesha njia nyingine mwanamke itakayomkomboa badala ya kukaa nyumbani mwisho wa siku atajifunza ujasiriamali kupitia biashara ya Kanga.
Mfumo wa shindano lenyewe utakuwa kama ifuatavyo:
Wasikilizaji wa E fm ambao ni wanawake wanakaribishwa kushiriki shindano la kubuni maneno ya Kanga kupitia kipindi cha UHONDO na maneno hayo yawe na neno UHONDO .
“Mfano Uhondo wa Ngoma uingie Ucheze” na Mshindi atajinyakulia kitita cha Shilingi za Kitanzania milioni moja
Hata hivyo shindano hilo halitaishia hapo, kwani baada ya kupata mshindi neno lake la Ushindi zitatengenezwa kanga zitakazoandikwa neno hilo ikiwa ni hatua ya pili sasa ya kumwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi.
"Zikishatengenezwa kanga hizo, Efm kupitia kipindi hicho cha Uhondo, itatatoa nafasi kwa wanawake kutengeneza pesa na kujikwamua kwa kuuza Kanga hizo na Mwanamke yoyote hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani atachukua kanga hizo na kuziuza ambapo kwa kila doti moja ya kanga atapata asilimia 30% ya pesa.
“ Ndugu zangu waandishi wa habari naomba kusisitiza tu hapa kuwa shindano hili litashirikisha wanawake pekee”. Alisema Dina Marios
Mkurungenzi wa Mawasiliano wa( EFM) Denis Ssebo akizugumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Wasikilizaji wa E fm ambao ni wanawake wanakaribishwa kushiriki shindano la kubuni maneno ya Khanga kupitia kipindi cha UHONDO na maneno hayo yawe na neno UHONDO . “Mfano Uhondo wa Ngoma uingie Ucheze” na Mshindi atajinyakulia kitita cha Shilingi za Kitanzania milioni moja. Kulia ni Mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Uhondo wa EFM Dina Marios leo Jijini Dar es Salaam
Mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Uhondo wa EFM Dina Marios zungumza na waandi wa habari hawapo pichani kuhusu shindano hilo leo Jijini Dar es Salaam
Wanahabari wakimsikiliza kwa makini Mkurungenzi wa Mawasiliano wa
(EFM) Denis Ssebo leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...