Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli,akiwahutubia Wananchi wa Tabora jioni ya leo
kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi.Dkt Magufuli alisema kuwa Serikali
yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye
wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi
nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe
mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo
amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.
Sehemu
ya umati wa watu waliokuwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya
leo walipokuwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini
na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania
kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25
mwaka huu.

Mgombea
wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi
Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tabora waliofurika
kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia anataka kujenga
Tanzania mpya yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
Mmoja
wa Makada walioko kwenye timu ya uhamasishaji wa kampeni za
CCM,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa Tabora kwenye mkutano wa
kampeni za Urais ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi
(CCM),Dkt John Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa mji wa Tabora
waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Ali Hassa Mwinyi mapema leo
jioni,alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa
wananchi wa mji wa Tabora waliojazana kusikiliza Sera na Mipango ya
Chama Cha Mapinduzi itakayotumika kuongoza kwa miaka 10 ijayo.
Wananchi wakishangilia .
Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John
Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa
hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora.
CCM endeleza kampeni na sera za maendeleo.
ReplyDelete