Ni jambo lilo wazi kuwa watu wote hawawezi kuwa sawa, hivyo watu wote hawawezi  kuwa matajiri. Hivyo kulipo na matajiri  wakubwa na  maskini nao ni wengi. Kwa sababu tajiri na maskini wanategemeana.  Utajiri hauwezi kuwepo bila kuwepo umaskini.Kwa mantiki hiyo ili tajiri awepo maskini lazima awepo na   maskini akiwepo  na tajiri atakuwepo, wote wanategemeana. Kanuni hii ni kwa watu na hata nchi.
Ni kweli matajiri wanachukia umaskini  na maskini wenyewe wanatamani utajiri. Hivyo si rahisi kwa tajiri kupenda  maskini awe tajiri.Kwani maskini akiwa tajiri  utajiri wake unakuwa mashakani. 
Hivi karibuni nimesikia kauli za  wagombea uongozi katika taifa letu wakisema wanauchukia umaskini, kitu ambacho ni kizuri, na kwamba wanatamani watu wote wawe matajiri. 
Hapo ndipo nilipopata ukakasi, je hawa wagombea wanalizungumzia jambo hili kwa dhati, wanaelewa kweli miiko na taratibu ya vitu mbalimbali kutegemeana katika maisha? Lakini nikijaribu kuwaangalia wao binafsi, je  ni matajiri au maskini. 
Kama maskini wanaweza kulizungumza hili kwa dhati  na wangependa na wao wawe matajiri. Lakini kama wao ni matajiri, basi hapo tunaogepewa kwani hakuna tajiri anayependa maskini awe tajiri kama yeye. Watanzania tutafakari.
R. Kahwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kama vyote hivyo vinategemeana (Umaskini na Utajiri), basi kwa mtazamo wangu, naona ifike wakati binaadamu tujuwe 'kukina/kutoshekai' na kusema na nafsi zetu, pengine itasaidia kutokuwa na tamaa ya kutaka kumiliki kila kitu ilhali uwezo mdogo au hauruhusu kabisa! Hata hao wagombea kuna matajiri na bado wanataka zaidi, kuna maskini na wao pia wanapigania kuwa matajiri na kuna waliosalia ni zaidi ya umaskini, maana hata kimaoni au kimaamuzi hawana sauti wala nafasi yeyote katika jamii ya kusikilizwa ama kukidhiwa matakwa yao in any aspect of life. Isipofikia hivyo basi chuki ya tajiri kwa maskini itazidi kuimarika.

    ReplyDelete
  2. Umasikini wa hali na kipato siyo kitu cha kujivunia ni hali ambayo inatakiwa kuondolewa katika jamii zetu. Ndiyo maana umasiki ulikuwa kati ya maadui watatu ikiwemo ujinga na magonjwa tulioamua kama nchi kupigana ili kuuondoa nchini, Katika nchi zetu zenye madeni mengi ya nje na ndani na mapato yasiyokuwa makubwa ya kuweza kukidhi mahitaji yote, kumaliza ufukura kwa haraka si rahisi kama wanasiasa wanavyozungumza. Hata baadhi ya ahadi zinazotolewa watu wenye uelewa wanauliza hivi hawa wanasiasa hela watazitoa wapi. Ila nia ikiwepo ya kutafuta njia mbadala za kukusanya fedha kuondoa rushwa kabisa na kutumia mapato ili kuinua maisha ya wananchi ikiwemo wa vijijini nchi yetu itapunguza sana umasikini wa kipato na hali za maisha duni zilizopo.

    ReplyDelete
  3. Matajiri wakiwekeza katika viwanda na biashara wanaweza kuongeza ajira inayoweza kuchangia kupunguza umasikini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...