Blogger mpiganaji wa Bukoba Faustine Ruta anapenda kumshukuru Mungu kwa kumfikisha leo hii Sept. 24, siku yake ya kuzaliwa. Anasema hakika Mungu ni mwema kwa kila jambo. Anaishukukuru familia yake, ndugu, jamaa, marafiki na majirani kwa kumsindikiza vyema katika safari yake hii ya maisha.
"Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuishuhudia siku hii. Ni neema kubwa. Hakika napaswa kutambua kwamba kila siku katika maisha yangu ni dhamana ambayo natakiwa niitumie kwa mambo mema", Faustine amesema katika mahojiano maalumu na Globu ya Jamii usiku huu.
Akaongeza: "Napenda kuchukua fursa hii pia kuwashukuru wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki kunisapoti kwa mambo mbalimbali ili mradi nifikie pale ambapo waliamini ni sehemu bora zaidi katika maisha yangu mpaka sasa.
"Niwashukuru MABLOGGER wenzangu wote wa Tanzania Bloggers Network (TBN) kwa ushirikiano tulionao", alimalizia.
Globu ya Jamii, ambayo inafanya kazi kwa karibu sana na Faustine, inamtakia maisha mema na yenye mafanikio mpiganaji huyu mchapakazi na mbunifu. Tunajivunia kuwa naye pamoja...
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...