Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu
Abdallah Bulembo ambaye pia ni Kiongozi wa msafara wa kampeni za Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi
CCM,akiwaongoza baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama hicho na wageni waalikwa kutoka Serikali
ya Mkoa wa Geita kukata Ndafu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu
ya Eid El Hajj kwa pamoja,wakati wa mapumziko ya shughuli za kampeni za
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,ambapo leo alitarajia
kuendelea na kampeni zake mkoani Shinyanga.
Wakati huo huo Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama
Cha Mapinduzi CCM Dr.John Magufuli ameahirisha mikutano yake ya kampeni
aliyokuwa aifanye leo Mkoani Shinyanga ili kupisha sikukuu ya Eid El
Hajj,pia amewatakiwa Watanzania wote popote pale walipo sikukuu njema na yenye Baraka mbele
za Mwenyezi Mungu na na kuwa tuendelee kuidumisha Amani ya Nchi yetu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
CCM,Ndugu Abdallah Bulembo ambaye pia ni Kiongozi wa msafara wa kampeni
za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitia chama cha
Mapinduzi CCM,akizungumza jambo mbele ya baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama hicho
na Serikali ya Mkoa wa Geita wakati wa mapumziko ya
kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj kwa pamoja,mapema leo mchana mkoani Geita.
Ndafu akiwa ameandaliwa tayari kwa kuliwa.
Ndafu ikikatwa kwa pamoja.PICHA NA MICHUZI JR-GEITA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...