Aliyekuwa Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard (Kulia) akifungua mkutano mkuu wa IPC jana katika ukumbi wa Maktaba ya Iringa katikati ni Daud Mwangosi ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa IPC akifikiri jambo.
Aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi (kushoto) akihojiwa na mzee wa matukio daima Bw Francis Godwin  ambaye alikuwa ni katibu msaidizi wa IPC juu ya wanahabari kudumisha umoja na mshikamano wakati wa uhai wake.


Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa cha chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi tarehe Kama ya leo miaka mitatu iliyopita aliuwawa  katika vurugu za Polisi  na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa .
Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .
Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...