Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli aliyenyanyua kofia (katikati) akiwasili
katika uwanja wa CCM mjini Bariadi kwa ajili ya kuwahutubia kwenye
mkutano wa kampeni mkoani Simiyu.
Wananchi wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi
Wananchi
wa Nanga wilaya ya Itilima wakishangilia ujio wa Mgombea Urais wa
CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia
Umati
wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika
kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya leo
Wananchi
wakimsiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufui alipokuwa
akiwahutubia mjini Meatu jioni ya leo.Dkt Magufuli leo ametembelea
wilaya ya Busega,Bariadi,Itilima pamoja na wilaya ya Meatu mkoa wa
Simiyu
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,
Dk.Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Mwanhunzi jioni ya leo mjini
Meatu mkoani Simiyu,Dkt Magufuli alisema kuwa atakapokuwa Rais atakuwa
karibu na wananchi wanyonge na kuwa yeye anatoka katika familia ya watu
maskini na anajua nini maana ya umaskini,Alisema anatoka kwenye familia
ya wakulima na wafugaji hivyo anajua nini ambacho anatakiwa kufanya
kuboresha maisha ya makundi hayo mawili na kwenye hilo atahakikisha
anaweka mazingiza mazuri ya matumizi bora ya ardhi.

Alisema Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.
"Nitakuwa upande wenu wananchi wanyonge.Serikali yangu ni marufuku watu wa bodaboda kushikwa na polisi.Serikali yangu haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo.Hivyo sitakuwa tayari kuona mama ntile wanatozwa kodi.Najua nitaimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yangu lakini nitawabana wafayabiashara wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi,"alisema Dk.Magufuli.
Aliwataka wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.
Dk.Magafuli aliweka wazi anapenda mabadiliko yenye tija na kwamba Serikali yake itasimamia nidhamu kwa watumishi wa umma ili wafanye kazi ya kuwatumikia waanchi usiku na mchana na ndio maana atawalipa vizuri na kuongeza hapendi watu wavivu kwenye kazi.

Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa
wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu
jioni ya leo.
Wananchi wa Mwanhunzi mjini Meatu wakifuatilia mkutano huo wa hadhara wa kampeni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...