Kocha wa Timu ya Mbeya City fc a.k.a Wakoma Kumwanya ndugu,
Juma Mwambusi akizungumza jambo na baadhi ya Vyombo vya Habari mara
baada ya Mtanange huo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika
katika Uwanja wa kumbukumbu Sokoine Jijini Mbeya, Ambapo Mbeya City FC waliibuka kidedea kwa kuichalaza Jkt Ruvu goli 3-0, ambapo Dakika ya
23 mchezaji Joseph Mahundi kuipatia Mbeya City Goli la Kwanza na Goli
la Pili toka kwa Temy Felix Dakika ya 57 kwa mkwaju wa Penati, huku
Goli la Tatu kufungwa na David Kabole Dakika ya
71.
kiungo wa Mbeya City fc Geofrey Mlawa akiteleza na Mpira
katika Mtanange huo uliochezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini
Mbeya.
Kamati ya Ufundi..
Baadhi ya Mashabiki Kinazi wa Timu ya Mbeya City FC wakishangilia katika Mtanange huo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, ambapo Mbeya City waliibuka mshindi kwa goli
3-0...
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...