Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla leo mchana ameaga rasmi watumishi wa Wizara ya Maji na kwenda kuanza majukumu mapya kama Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
 Mhe. Makalla ambaye alifika Wizarani hapo, akitokea Ikulu alikoapishwa rasmi na Mhe. Rais, Jakaya Mrisho Kikwete, mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. 
Mhe. Makalla ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maji kwa zaidi ya mwaka mmoja, aliweza kufanya kazi kwa weledi mkubwa licha kuwa mgeni kwenye Sekta hiyo, ambapo aliweza kuzunguka karibu mikoa yote na kutembelea karibu Mamlaka zote za Maji nchini katika kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi ya maji.
 Mhe. Amos Makalla akisalimiana na watumishi wa Wizara ya Maji waliompokea mara baada ya kuwasili Wizarani, pamoja na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Gideon Manambo.
 Mhe. Amos Makalla akiwa ofisini kwake, alipofika kuaga Wizara ya Maji.
 Mhe. Amos Makalla akipokea shada la maua kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Beatrice Patrick.
 Mhe. Amos Makalla akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maji, wakati akiaga wizarani hapo.
Mhe. Amos Makalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara ya Maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...